Unaweza ukajitetea sana jinsi ambavyo hali ni ngumu.
Unaweza ukajitetea sana jinsi ambavyo huwezi kufikia malengo na ndoto zako lakini ukweli unabaki kwamba hizo sababu na kujitetea hakukubadilishii hali uliyonayo.
Uchumi umekua mgumu sana unaweza kutumia hiyo kama sababu ya kujitetea au kama fursa ya kutafuta suluhisho.
☹ Hata Mungu hataki watu wanaojitetea na kutoa sababu kwanini hawawezi na kwanini wamekosea. Kaa kwenye nafasi yako utatue matatizo yako.
Ifanye akili yako ifikiri. Akili ikishindwa kutumika vyema itatumika vibaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni