Jumamosi, 30 Julai 2016

AMKA

��Morning Rise Up��

✍��SABABU KUMI ZINAZO KUFANYA USISONGE MBELE

Wakati tukikuta mambo yetu hayaendi huwa tunadhani kuna mchawi anaiingilia mambo yetu kumbe mchawi wa mambo yetu ni sisi wenyewe  na si vinginevyo .

Zifuatazo ni sababu kumi zinazokufanya usisonge mbele :

1.Huna ndoto : Kama hujui unataka nini katika maisha yako wewe utakuwa ni mtu wa kusubiri Jua lichomoze na kuchwa .Hutakuwa na msukumo wa ndani wa kuhakikisha kuwa siku moja ndoto yako inakuwa kweli .Umekuwa ukifanya vitu kwa mazoea kwa sababu huna ndoto yoyote inayokufanya kuwaza kila siku namna gani utaifikia.

2.Unawasikiliza watu sana kuliko kujisikiliza mwenyewe:Maisha yako ni yako na si ya kaka yako wala mjomba wako au ndugu yeyote na rafiki yeyote uliye naye . Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe(Every body will carry his own burden).Kama unaamini katika unachokifanya na unajua kitakufikisha mahali endelea kufanya kadri unavyoweza .Watu wengi si wazuri na hawajui unakokwenda japo wanaweza kujua ulikotoa .

3.Hutafuti Maarifa : Bila maarifa hutaenda kokote na maisha yako hayatabadilika .Utakuwa kama mtu anayepiga ngumi ukutani ambapo mwisho wa siku huumiza mkono wake mwenyewe .Kama siyo msomaji wa vitabu ,kuperuzi kwenye mtandao kutembelea blog kama www.kijanajithamini1.blogspot.com na www.maishanamafanikio.blospot.com hautaweza kupata maarifa ambayo yatakufanya ufanye mambo yako kwa uwaredi mkubwa na kwa tofauti .Utakuwa ni mtu wa kufanya mambo kimazoea maana huna maarifa na mwisho wa siku hutatoka pale ulipo.

4.Unajihurumia sana : Umekuwa mtu wa kujihurumia sana na kutaka kukaa kwenye comfort zone ,sehemu ambayo unapata vitu kwa urahisi .Hutaki  kuumiza kichwa na kuwaza juu ya maisha yako .Umekuwa mtu wa kutaka vitu ambavyo vimeshafanywa na wenzio maana hutaki kuteseka  na kukutana na changamoto .

5.Unaishi kwa yaliyopita : Maisha siyo jana maisha ni kesho .Kama ukiangalia ulivyoshindwa jana hutafikiria kuhusu kesho .Ukiangalia biashara ya jana ilivyodhurumiwa na kuibiwa hutafanya biashara kesho .Acha kabisa kuishi kwa ya jana hutasonga mbele .Angalia sana kesho yako , Maisha ya watoto wako wa kesho ,mahusiano na familia yako ya kesho na si vinginevyo .

6.Huchukui hatua : Umekuwa mtu wa kusema nitafanya kesho na kesho ikifiika hufanyi .Umekuwa na mipango mingi isiyokuwa na utekelezaji .Kama huchukui hatua utabaki hapo hapo ulipo  hakuna jambo jipya litakalotokea .

7. Unasubiri Matokeo ambayo hujafanyia kazi ; Usitegemee muujiza .Kile apandacho mtu ndicho atakachovuna .Unawezaje kuvuna mahali ambapo hujapanda??? Hey ! Unawezaje kuvuna maharage kwenye shamba la mahindi???? .Newton anasema ili kazi ifanyike lazima kani (force) itumike na umbali(distance ) uwepo .Hakuna matokeo yasiyosababishwa.

8.Huzalishi mawazo : Umekuwa mtu ambaye hutaki kuwaza kwa mtazamo mpya na kuzalisha mawazo mengi kadri iwezekanavyo .Umeishi kwa wazo la mwaka 1999 mpaka leo na hujui kama dunia imebadilika .Hey! Amka anza kuzalisha mawazo .

9.Umeishi kwa tahadhari nyingi :Kila kitu kwako umechukua tahadhari ,unahisi ukianza biashara fedha zako zitapotea ,unahisi ukianzisha kitu hakitasonga mbele .Kwanini umekuwa hivo (too cautious) ????.Kama hutaachana na tabia hii hutatoka mahali ulipo na kamwe usitafute mchawi .

10.Hujifanyii tathimini :Huna tabia ya kupima yale uliyoyafanya kwa siku,wiki,mwezi na mwaka na hivyo unahisi kama unaenda mbele kumbe unarudi nyuma .Ni muhimu ukawa na tathimini ya mambo yako binafsi.

JITATHMINI...

Ijumaa, 29 Julai 2016

NJIA ZA MAFANIKIO

TAMBUA NJIA ZA MAFANIKIO.

Natumaini hujambo,msomaji wa makala hii.Leo tutazungumza njia za mafanikio ktk maisha yetu ya kutafuta.

Mafanikio yapo mengi,kuna mafanikio ya kibiashara,kielimu,kijamii na kisiasa yote yanaongozwa na mbinu zifuatazo kwa kutawaliwa na utayari wako.

~KUJITAMBUA,jitambue wewe ni nani,unafanya nini,jamii inanufaika kwa uwepo wako? walio wengi bado hawajajitambua kutokana na mfumo wa maisha ya jamii unayoishi wengi wanafikiri kujitambua baada ya umri kua umetupa mkono.Ni lazima utambue uwezo wako ktk kupambanua mambo ya mafanikio na utambue jinsi gani utaweza kuisaidia jamii kutokana na kujitambua kwako,Hivyo anza leo kujitambua wewe ni nani,kwanini unaishi hivyo? Unaonaje jamii ikinufaika kwa kujitambua kwako?

~JITOFAUTISHE,mara baada ya kujitambua sasa anza kujitofautisha kutoka makundi ya watu wasio jitambua kwasababu unapoendelea kuchangamana nao utakua hujabadili kitu,utakapokua umejitofautisha sasa wenzio wataiga mfano wako hata wasipo kuambia lakini utaona tu,kumbe kwa kujitambua kwako na kujitofautisha kwako tayari utaokoa maisha ya wengi ambao walikua wameanza kupotea.Tayari utaanza kuisaidia jamii kutokana na kujitofautisha kwako.

~TAFUTA KITU CHA KUKUUNGANISHA NA JAMII YAKO,unaweza kutafuta shughuli itakayo kuunganisha na jamii yako.Kwa mfano tafuta biashara itakayogusa maisha ya jamii kutokana na huduma utakazo toa,tafuta kazi ambayo itakukutanisha kila siku na jamii yako,unaweza kukutana na jamii kwa njia nyingi ambapo kwa njia hizo itakusaidia wewe kubadili maisha ya wengi kuanzia mitazamo hadi uhalisia wa maisha yao ya kila siku.

~KUMBUKA KUJALI MUDA,mara nyingi muda ndio kila kitu kwako katika kukamilisha safari ya mafanikio utaamua mwenyewe kwa muda gani ufikie kilele cha mafanikio,inapendeza sana kuwa mtu wa kujali muda hasa kutumia muda kwenye shughuli za mafanikio.Umri sio rafiki kumbuka leo ni yako na sio kesho tunza muda uvune matunda yake.Sio lazima ushinde kazini au kwenye biashara lakini tambua hata sekunde moja kwako ni mali kwasababu unaweza kuamua kufanya kitu kizuri cha kubadili maisha yako iwe kwa mtazamo au uhalisia.

~TAMBUA MCHANGO WA MARAFIKI,marafiki wanaweza kubadili maisha yako kua mazuri sana,mazuri kiasi,mabaya na mabaya sana.Hivyo chunguza kundi la marafiki zako utaelewa maisha yako huenda umezungukwa na marafiki wanao kukatisha tamaa ya kufanya jambo zuri la manufaa,huenda umezungukwa na marafiki wanao kushauri vizuri lakini hawako tayari kukusaidia kufikia ndoto zako,huenda umezungukwa na marafiki wanao kupeleka mitandaoni kuzurura,huenda umezungukwa na marafiki wanao furahia kushindwa kwako.Amka ndugu ni kheri rafiki mmoja mwenye akili kuliko rafiki mia moja wapumbavu uwingi wao utakua kama makelele katika maisha yako kwasababu hamna jipya mtakalo shauriana na kulitendea kazi.

~TIMIZA MALENGO YAKO,unapokua tayari umepata shughuli ya kufanya jitahidi kuchunguza kwa undani kama shughuli hiyo inaweza kukutimizia malengo yako ambayo mengine ni ndoto za mafanikio unazo tamani kuzitimiza na kuziishi.Shughuli unayoifanya ndio inakujengea uhakika wa ndoto zako,usifanye shughuli inayokupa pesa ya kula tu na kuvaa,au kununua mafuta ya gari halafu ukarizika tafuta shughuli inayoweza kudumu kwako na kizazi chako nina maana kua utapokua mzee au umekufa wanao wajivunie jitihada zako za kuwakomboa kutoka umasikini,Hivyo malengo lazima yawe makubwa ili uongeze nguvu ya utafutaji,Kamwe usiweke lengo unalolizidi bali weka lengo linalokuzidi ili kulifikia uelewe unacho fanya na utajipima utendaji kazi wako.Hakikisha malengo yako yanatimia kwako na kizazi chako.

~UTAYARI WA KUSAIDIWA,usiwe mjuaji sana utakosa watu wa kukusaidia badala yake jishushe uelimishwe na usaidiwe ili uweze kufanya shughuli inayoweza kudumu kwako na kizazi chako,Ujuaji mwingi ni sumu kwa upeo wako kwasababu huenda unacho kijua hakina msaada kwako,jitahidi kua tayari kusaidiwa na wenzio katika mambo ya mafanikio.

JIFUNZE KUMTOLEA MUNGU,Mungu wetu anajaribiwa kwa sadaka na sio kitu kingine jiulize tangu uanze shughuli za kutafuta mafanikio umewahi kumtolea Mungu ile kumi ya mavuno? au hata sadaka umewahi kutoa? kutoa ni moyo unapotoa Mungu anarudisha mara kumi hivyo usiwe mchoyo hadi kwa Mungu,na unapotoa epuka kujitangaza wengi wanakosea akitoa sadaka basi anataka mtaa mzima wamuelewe,sadaka yako na iwe siri kati yako na Muumba wako.

Natumaini umepata wazo jipya kuhusiana na siri za mafanikio.Kwa ushauri wa kukusaidia shughuli za kufanya ufikie ndoto zako tuwasiliane��������

WhatsApp ……0673214813………

Alhamisi, 21 Julai 2016

Jumatano, 20 Julai 2016

JINSI DAKIKA MOJA INAVYOWEZA KUBADILI MAISHA YAKO.

Duniani kote,kila mtu ana miliki masaa 24 katika masaa hayo tunamgawanyiko mara tatu yani masaa 8 ya kufanya kazi,masaa 8 kulala na 8 kufanya shughuli za ziada.Tunapozungumzia muda ni dhahiri kua wengi wametawaliwa na muda badala ya wao kutawala muda.

unaweza kua unajiuliza ni kwa namna gani?

sasa sikiliza,kama wewe ni muajiriwa au umejiajiri mwenyewe unatakiwa kufuata utaratibu huu ili uweze kumiliki muda na sio muda ukumiliki.

>Panga ratiba yako ya shughuli za kila siku ambazo zinakuingizia kipato,Unapofanya shughuli bila ratiba ni wazi kwamba wewe si mwaminifu kabisa kwasababu hapo katikati anaweza kuja rafiki akakubeba mwende matembezi na ukakubali,inakua hivyo kwasababu huna ratiba yani wewe ni kanyaga twende.Sikiliza ratiba yako ndio inaamua wewe uwe mtu wa namna gani,hivyo ratiba huendana na muda.Unaona dakika moja ya kumkubalia rafiki mwende matembezi itakugharimu sana kuifidia kwasababu pengine ungebaki kwenye shughuli zako usingepata majanga ya kuibiwa au kuumizwa kutokana na majanga ya matembezi.ILINDE DAKIKA YAKO

2.Andaa muda wa kujifunza vitu vya mafanikio,watu wengi hawana muda wa kujifunza tangu alipo maliza chuo au form four hajawahi kujifunza tena.Elimu haina mwisho ndugu yangu labda nikupe siri moja wenzetu wazungu kwa siku wanatenga masaa 2 tu ili kujisomea vitabu au makala mbalimbali ambazo zinalenga kuwaongezea ujuzi ktk maisha.Ajabu huku kwetu Tanzania watu mko bize kusoma comments za matusi kwa wema sepetu,mko bize kutazama ngono,mko bize kujifunza ujambazi yani mambo yasiyo faa kabisa.Hebu tumia hiyo dakika moja kuilisha akili yako busara na maarifa ya maisha,halafu uone dakika hiyo itakavyo kubadili kabisa wewe utajikuta ni mtu mwenye utofauti na wale wasio na muda wa kujifunza.

SIRI ZA MAFANIKIO

��Morning Rise Up��

✍��JIFUNZE SIRI HIZI ZA WATU WALIOFANIKIWA

��Ili ufanikiwe hupaswi kufanya kila kitu .Unapaswa kuwa makini kujua kipi unapaswa kufanya na kipi hupaswi kufanya .Jumatano hii tulivu nataka nikuuleze mambo ambayo watu waliofanikiwa huwa hawayafanyi .

���1.Hawaishi kwa  yaliyopita .��
Watu waliofanikiwa huwa wanaishi kwa methali uliyofuundishwa na mwalimu wako kuwa yaliyopita si ndwele tugange yaliyopo na yajayo .
Kamwe usifikirie mambo yaliyopita ,iwe ni biashara iliyoharibiwa ,iwe ni kazi au mahusiano huwa yanaumiza na kushusha morali  ya kusonga mbele .Shida ni kwamba ukifikiria sana yaliyopita huwezi kufanyia kazi ndoto yako .Ni vizuri sana kujua maisha ni leo lakini hasa  kesho na si jana .Kwanini unakumbuka ulivyoshindwa jana ??? kwanini unakumbuka mahusiano yaliyoovunjika???

Unapaswa kujua kuwa lililoshindikana jana leo linaweza kufanyika kwa uzuri na uwaredi mkubwa sana .Mwimbaji mmoja wa Nyimbo za injili katika Albamu yake moja anasema "Jana imepita ,leo ni siku mpya tengeneza njia yako ili Bwana atende ".

���2.Hawafanyi kisichoendana na ndoto zao ��
Watu waliofanikiwa huwa kabla ya kufanya huwa wanajiuliza maswali kama haya : kwanini nifanye hiki au kile?? je kinafaa??  je ni sahihi kwa mazingira haya ???

Rafiki kama unataka kufanikiwa hupaswi kufanya kila kinachokuwa mbele yako .Ni muhimu kujua kitakusaidia nini pindi ukikifanya na utakosa nini usipofanya .

���3.Hawaamini kuwa unaweza kumfurahisha kila mtu��
Huwezi kumfurahisha kila mtu kwa kile unachofanya .Watu waliofanikiwa wanalijua hili .Ni muhimu sana kujua kuwa hapa dunia watu wote hawawezi kukufurahia na hivyo usifanye vitu kwa kuwafurahisha watu .Fanya lile liloko moyoni mwako na ndani ya uwezo wako kama kweli unataka kufanikiwa .

���4.Hawaamini kuwa kuna mtu hakosei ��
Watu waliofanikiwa huamini kuwa ili ufanikiwe lazima ukosee na makosa ni sehemu ya kujifunza .Hakuna mtu ambaye amekamilika .Hujifunza kutokana na makosa yao ya kila siku na kupitia makosa hufanya makubwa.Ili ufanikiwe usiogope kukokosea maana kukosea ni sehemu ya maisha.

���5.Hawaachi kujiuliza kwanini wako hapo walipo ��
Watu waliofanikiwa mara zote hupenda kujiuliza ni kwanini wapo hapo walipo na hii ndo tofauti kubwa kati ya watu waliofanikiwa na wale ambao hawajafanikiwa.Watu waliofanikiwa hujiona kuwa wao siyo tu waliosababisha kufika pale walipo katika mafanikio hata kama wametumia nguvu zao wenyewe kufanikiwa .Lakini pale waliposhindwa kitu waliamini wao ndio sababu ya kushindwa kwao bila kumlaumu mtu mwingine .

���6.Hawaachi Kuona Picha kubwa ya maisha yao ��
Watu waliofanikiwa huamini kuwa picha kubwa ndiyo pekee inayowawezesha kufanya mambo makubwa na kufanikiwa .Kila siku wanawaza mambo makubwa.Hawaangalii walipo sasa na wana nini lakini huangalia mambo ya mbele sana .✍��Ni muhumu sana ukitaka kufanikiwa usiangalie pale ulipo leo lakini uweke picha kubwa kichwani mwako kuwa unaweza kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa.Kwanini unaangalia umaskini wa familia yako??? kwanini unaangalia mazingira??? .

���7. Hawaachi Kuvumilia shida ya muda kwa faida ya miaka mingi .
Watu waliofanikiwa huwa huwa hawakwepi maumivu ya muda .Wao ni wavumilivu  sana tofauti na maskini ambaye hutaka kufanikiwa haraka au kufurahia raha ya muda mfupi .

Ndugu kama una nia ya dhati ya kufanikiwa ni muhimu sana ukawa mvumilivu katika mambo unayoyafanya .Acha kutafuta raha ya muda mfupi huku ukijiua mwenyewe .

Kwa maarifa zaidi tembelea blog hizi
www.josinahleonard.blogspot.com

Jumatatu, 18 Julai 2016

SAYANSI YA KUSINYAA NA KUSIMAMA KWA UUME(NGUVU ZA KIUME)

*SAYANSI YA KUSIMAMA NA KUSINYAA KWA UUME*
(Yaani Sayansi ya Nguvu za Kiume)

*UTANGULIZI*
Kwanza kabisa naamini kuwa wote hapa ni watu wazima na hivyo tutajifunza jambo hili kama watu wanaojielewa.  Pili Lengo kubwa la mafunzo haya ya kila wakati ni kuwa na uhakika wa afya zetu sisi wenyewe na watu wa familia zetu pamoja na kupata ufahamu mkubwa ili kuweza kuwadadavulia wateja wetu pindi tutakapohitajika kufanya hivyo.  Kwa hiyo ni vema kujifunza kwa umakini na kujitahidi kurudia rudia kusoma ili uweze kuelewa vizuri. Na siku nyingine wewe utawafundisha team yako. Kumbuka bila maarifa timu yako itakufa bila wewe kujua. 

*SASA TUENDELEE....*

*I.*  *SUALA LA UKOSEFU AU UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME*

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume DUNIANI.

*Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  basi?*

Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni *ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu*

*KUSIMAMA KWA UUME (ERECTION)*

Kuna hatua  mbili  Muhimu  katika  Kusimama  kwa  UUME.

Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo:

1. Hatua  ya  KWANZA

Ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari.

2. Na  hatua  ya  pili

Ni lazima, uume  wake  *uendelee  kusimama*  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION. Yaani ana nguvu kamili za kiume.

*II.* *JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA*

Jinsi  hatua  za  kusimama  kwa  uume zinavyotokea

1. HATUA YA KWANZA:

DAMU  KUTIRIRIKA  KWA  KASI KUINGIA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME  NA  KUUFANYA  UUME  KUSIMAMA  NA  KUWA  MGUMU.

Mwanaume anapopata  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, mishipa  ya  fahamu iliyopo  kwenye  ubongo,  hupeleka  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo, ambayo  nayo  hupeleka  taarifa  hadi  kwenye  mishipa  ya  uume. 
  
Taarifa  inapofika  kwenye  mishipa  ya  uume  huifanya  mishipa hiyo  ku-relax  na  hatimaye   kufanya  mishipa  ya  ateri  kufunguka  na  kutanuka. Mishipa  ya  ateri  inapo  tanuka  na  kufunguka, huruhusu  damu  kuingia  kwa  kasi  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  huume  kusimama.

Ni  muhimu  kujua  kuwa, mishipa  ya  uume  inapo relax  hupelekea  kuisukuma na  hatimaye  kuiziba  mishipa  ya  vena  iliyo  karibu  na  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuiondolea  uwezo  wa  kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  sehemu  nyingine  za  mwili.

N.B: Kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika  sehemu  nyingine  za  mwili.  Au  kwa  lugha  nyingine  unaweza  kusema, kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kuhakikisha  hakuna  damu  kwenye  mishipa  ya  uume.

2. HATUA  YA  PILI  :

DAMU  KUENDELEA  KUHIFADHIWA  KATIKA  UUME  WAKATI  UUME  UKIWA  UMESIMAMA  NA  HIVYO  KUUFANYA  UUME  UENDELEE  KUDUMU  KATIKA  TENDO LA NDOA   KWA  MUDA  MREFU.

Uume  ulio  simama, ili  uendelee  kusimama, ni  lazima  mishipa  ya  vena  isiwe  na  uwezo   wa  kunyonya  damu  kutoka  katika  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika  sehemu  nyinginezo  za  mwili.

Mishipa  ya  Vena  ndio  inayo  husika  na  kunyonya damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume na  kupeleka  sehemu  nyingine  za  mwili.  Ili  uume  uendelee  kusimama  lazima  mishipa  hii  ya  vena  iwe imezibwa. Ili  iweze  kuzibwa   ni  lazima  misuli  laini  ya  kwenye  uume  iwe - ime  relax na  hivyo  kuifanya  mishipa  ya  vena  kushindwa  ku  nyonya  damu  kutoka  kwenye  uume.

Endapo  mishipa  ya  vena  itazibuka , basi  itanyonya  na  kutoa  damu yote  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume uliosimama  na  kuipeleka  sehemu  nyinginezo  za  mwili  na  hatimaye  uume  huo ulio simama  na  utasinyaa  mara  moja.
[17/07/2016 18:43] Andrew: *III.* *JINSI  UUME  UNAVYO  SIMAMA  NA  KUSISIMKA*

Tumeisha  zifahamu  hatua  mbili  muhimu  katika  kusimama  kwa  uume

Jinsi  Uume  unavyosimama: Katika  uume  kuna chemba  yenye  mishipa  laini  sana, ambayo  ndio  huufanya  uume  kusimama.

Mishipa  hii  ipo kama  sponji  hivyo  huweza  kunyauka  na  kutanuka.

Damu  inapoingia  ndani  ya  mishipa  hii  huufanya  uume  kusimama  na  kuwa  mgumu  kama msumari (neno *msumari* ni mfano tu ili uelewe champion) ��������

Damu  inapoendelea  kuhifadhiwa  ndani  ya  mishipa  hii  wakati  wa  tendo  la  ndoa, huufanya  uume  uendelee  kusimama.

Mwanaume  anapopatwa  na  wazo la  kufanya  tendo  la  ndoa, mishipa  ya  fahamu  iliyo  kwenye  ubongo  hupeleka  ishara  kwenye  uti  wa mgongo, ambao  nao  hufikisha   taarifa  kwenye  mishipa  ya  uume.

Taarifa  ikisha  fika  kwenye  mishipa  ya  uume, huifanya  mishipa  ya  uume  ku-relax  na  mishipa  ya  uume  inapo  relax, hufanya  mambo  makuu  mawili;

i.  Kwanza  hufanya  mishipa  ya  ateri  kufunguka na  hivyo  damu  kutiririka  kwa  kasi  sana  kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume..
(Mishipa  ya  ateri  ndio  inayo  tumika  kama  njia  ya  kuingiza  damu  kwenye  uume. Bila  mishipa  ya  ateri  imara  na  yenye  afya, damu  haiwezi kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume, na  damu  isipoweza kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume, basi  uume  hauwezi  kusimama )

ii. Pili huibana  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuizuia    kunyonya  damu  kutoka  kwenye  uume  na  kuipeleka  kwenye  sehemu nyingine  za  mwili. Matokeo  yake  kuufanya  uume  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Kumbuka ,kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  neva  iliyo  karibu  na  mishipa ya  uume, ni kunyonya  damu kutoka  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  kwenye  sehemu  nyingine  za  mwili. Kwa  lugha  nyingine, kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kuhakikisha  hakuna  damu  kwenye  mishipa  ya  uume ulio simama.

Kadri  damu  inavyo  zidi  kuingia  ndani  ya mishipa  ya  uume, ndivyo  uume  unavyo  zidi  kuwa  mgumu  na  kukakamaa.

Na  kadri  damu  inavyo  hifadhiwa  ndani  ya  mishipa  ya  uume, ndivyo  uume  unavyo endelea  kusimama  wakati  wa  tendo  la  ndoa kwa  muda  mrefu.

Baada  ya  kumaliza  kufanya  tendo  la  ndoa, mishipa  ya  uume inarudi  katika  hali  yake  ya  kawaida (inanyauka ), ikisha  nyauka, mishipa  ya  ateri  inanyauka  pia, vena  zinafunguka  na  kunyonya  damu  katika  mishipa  ya  uume  na  kuirejesha  katika  sehemu nyinginezo  za  mwili  na  hatimaye  uume  kurudi  katika  hali  ya  kawaida (flaccid).

Hali  hii  itaendelea  kujirudia  kwa  kadri  utakavyo  kuwa  ukiendelea  kufanya  tendo  la  ndoa.

Mambo  Muhimu  Katika  Kuufanya Uume  Usimame na  Kuendelea  kudumu  katika  kusimama  kwa  muda  mrefu wakati  wa  tendo  la  ndoa.

*Sasa basi.... Ili  uume  uweze  kusimama  imara  kama  msumari na  uendelee  kusimama  imara  na  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo la  ndoa, ni  lazima  mambo  yafuatayo yawepo:*

1. Mishipa ya   uume iliyo  imara  na  yenye  afya  njema.

2. Mfumo   mzuri  wa damu  katika   mwili  mzima.

3. Mtiririko  imara  wa  damu kuingia  na  kutoka  ndani  ya  mishipa  ya  uume.

4. Ushirikiano  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  ya  kwenye  ubongo  (nerves), mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  mishipa  ya  kwenye  uume.

Ili  mwanaume  aweze  kuwa  imara  katika  tendo  la  ndoa, ni  lazima  mambo  manne  niliyo yataja  hapo  juu  yawe  sawa  sawa  bila  hitilafu  yoyote. Kinyume  chake, mwanaume  hawezi  kuwa  na  nguvu  za  kiume.
[17/07/2016 23:01] Andrew: *IV.* *MAMBO   YANAYO SABABISHA   UKOSEFU/UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.*

Tumeshajua   nguvu za  kiume  ni  nini, jinsi  uume  unavyo  simama, hatua  za  kusimama  kwa  uume, pamoja  na  mambo  yanayo  fanya  uume  uweze  kusimama  na  kuwa  na  uwezo  wa  kuendelea  kusimama  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Ni  vyema  tukajua  mambo  yanayo  sababisha  kushindwa  kusimama  kwa  uume, mambo  yanayo  sababisha  uume  ushindwe kuendelea  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa   pamoja  na  mambo  yanayo  fanya  mtu  ashindwe  kurudia  tendo  la  ndoa.

Yafuatayo  ni  mambo  yanayo  sababisha  ukosefu wa  nguvu  za  kiume.

*1.* *MAGONJWA YANAYOSHAMBULIA  MFUMO WA DAMU  PAMOJA NA MAISHA YA  DAMU.*

Damu  ndio  nishati  inayo wezesha  kusimama  kwa  uume  na kuufanya  kuwa  mgumu na  imara  kama  msumari.

Damu  ndio  nishati  inayo weza   kuufanya  uume uendelee kusimama  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Damu  ndio  nishati  inayo  upa  uume  uimara  na  uwezo  wa  kurudia  tendo  la  ndoa  zaidi  ya  mara  moja.

Hivyo  basi  ili  uume  uweze  kuwa  imara na  wenye  nguvu, pamoja  na  kuwa  na  uwezo  wa  kumudu  na  kustahimili   tendo  la  ndoa  wakati  wowote , basi  ni  lazima   mwanaume  awe  na mfumo  imara  wa  damu  utakao  ruhusu  kutiririka  kwa  damu  kwenda  katika  sehemu mbalimbali  za  mwili  ikiwamo  uume.

Ili  mfumo  uweze  kuwa  imara  ni  lazima  mhusika  awe  na  damu  ya  kutosha, na  pili  awe  na  mishipa  ya  damu  yenye  afya.

Katika  mwili  wa  mwanadamu,kuna  mishipa  inayo  tumika  kusafirisha  damu  kutoka  katika  sehemu moja  ya  mwili kwenda  katika  sehemu  nyingine  ya  mwili  ikiwemo  uume. Mishipa  hiyo  ni  kama  vile  vena (veins), atery ( ateri) na  capillary  ( kapilari )

Mishipa  hii  ya  damu  inapaswa  kuwa  imara  na  yenye  afya  njema  wakati  wote.   Mishipa  hii  ikipatwa  na  hitilifu, basi  itazuia  kusafirishwa  kwa  damu  katika  sehemu  mbalimbali za  mwili  wa  mwanadamu  na  hatimaye  kufanya  suala  la  kuwa  na  nguvu  za  kiume  kwa  mhusika  kuwa  ugumu  kwa  sababu   ya  kushindwa  kupeleka  damu  kwenye  mishipa  ya  uume.

Magonjwa  kwenye  mishipa  ya  damu  huzuia   kutirika  kwa  damu kwenye  ogani  muhimu   kama  vile  moyo, ubongo na  figo.

*VIASHIRIA  VYA  MAGONJWA  KWENYE  MISHIPA  YA  DAMU.*

Utajuaje  kwamba  una  magonjwa  kwenye  mishipa  yako  ya  damu ?

Ukiwa  una  matatizo  yafuatayo ya  kiafya, ni  ishara  kwamba, una  magonjwa  kwenye  mishipa  yako  ya  damu:

1.  Kolestrol ( Ama  lehemu  kwenye  damu )

Kolestrol  nyingi  kwenye  damu, huzuia  kutiririka  kwa  damu. Kolestrol  ikizidi  kwenye  damu,  hupelekea  kuziba   mishipa  ya  ateri  ambayo  kazi  yake  ni  kupeleka  damu  kwenye  uume. 
  
Matokeo  yake  ni  mhusika  kutokuwa  na  uwezo  wa  kusimamisha  uume  wake barabara  kwa  sababu uume  hauwezi  kusimama  bila  damu  kuingia  ndani  ya  mishipa  ya  uume.  
  
Hivyo  basi pamoja  na  kutumia bidhaa za nguvu  za  kiume, yakupasa  kutibu  kolestrol. Unaweza  kuondoa  kolestrol  kwenye  damu  kwa  kutumia  bidhaa zetu za kuondoa kolestrol. Jinsi  ya  kutatua shida ya  kolestrol  kwa  kutumia bidhaa zetu kama Arctic Sea na Argi Plus nk.

2.  Shinikizo  Kubwa  la  Damu

Shinikizo  Kuu la  Damu husababisha  mishipa  ya  ateri  ambayo  hutiririsha  damu  iingiayo  kwenye  uume  kuziba  na  kushindwa kutanuka  kwa  kiwango  inachotakiwa  kutanuka.

Pia  huifanya  mishipa  laini  katika  uume   kushindwa  ku-relax  na  hivyo  kushindwa  kuizuia  mishipa  ya  vena  ya  kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  kwenye  maeneo  mengineyo  ya  mwilini.

Matokeo  yake  kunakuwa hakuna  kiasi  cha  kutosha  cha  damu  iingiayo  kwenye  uume  na  hivyo  kufanya  uume  ushindwe  kusimama.

Vile  vile  hata  kiasi  kidogo  cha  damu  kinacho  ingia  kwenye  uume, kinashindwa  kuendelea  kuhifadhiwa  ndani  ya  uume  wakati uume  ukiwa  umesimama, na  matokeo yake  ni  uume  kusinyaa  ndani  ya  kipindi kifupi  sana  tangu  usimame.

Pamoja  na kutumia  bidhaa  za  nguvu  za  kiume, atapaswa   pia  kutumia bidhaa za kumsaidia mtu mwenye tatizo la  shinikizo  kuu  la  damu.

Kuna bidhaa za kusaidia mtu mwenye shinikizo kuu la damu ama pressure ya kupanda kama wengi wanavyoita.

3.  Ugonjwa  wa  kisukari :

Ugonjwa  wa  kisukari  ni  miongoni  mwa  vyanzo  vikuu  vya  tatizo  la  ukosefu wa  nguvu  za  kiume.  Kusimama  kwa  uume  kunategemeana  na  kutiririka  kwa  damu  mwilini. Kisukari  huathiri  mishipa  ya  damu pamoja  na  usambazaji  wa  damu  kwenye  ogani  muhimu  mwilini  kama  vile  moyo, ubongo, figo  na  uume.

Kiukweli, mwanaume  mwenye  kisukari  yupo  katika  risk  kubwa  ya  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume,m tena  katika  kiwango  kikubwa  sana.

Anashauriwa pamoja  na kutumia  bidhaa  za  nguvu  za  kiume, atumie  pamoja  na  bidhaa  mbalimbali kwa  ajili  ya  kubalance  sukari  yako mwilini. Kuna products za kumsaidia mtu wa kisukari. Kama huzijui uliza kwa upliner wako.

4. Magonjwa  ya  figo

Tatizo  la  ugonjwa  wa  figo  huathiri  vitu vingi  ambavyo  ni  muhimu  sana  katika  kuufanya  uume  uweze  kusimama  na  kuendelea  kudumu  katika  kusimama.

Tatizo  la  figo, huathiri  homoni, huathiri kutiririka   kwa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume. Huathiri  mfumo  wa mishipa  ya  neva  pamoja  na  nishati  ya  mwili mzima.

Pamoja  na  dawa  ya  kutibu  tatizo  la  nguvu  za  kiume, unapaswa  pia, kutibu  tatizo  la  figo. 
  
Kuna bidhaa za kuimarisha figo.

5.  Ugonjwa  wa  moyo

Moyo  ndio  supplier  mkubwa  wa  damu  katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili.  Ugonjwa  wa  moyo  hupunguza  uwezo  wa  moyo  kusambaza  damu  kwenye  mishipa  mbalimbali  ya  damu  na  hivyo  kuathiri  utendaji  kazi  wa  mishipa ya  damu  kama  vile  ateri  na  vena. 
  
Matokeo  yake  ni  mishipa  hiyo  kushindwa  kupeleka  damu  ya  kutosha  katika  uume  pamoja  na  kushindwa  kuifanya  mishipa  ya  uume  kurelax na  matokeo  yake,. Ukosefu  wa nguvu  za  kiume. 
  
Hivyo  basi, pamoja  na  products  za  nguvu  za  kiume, unapaswa  pia   kutibu  tatizo  la  moyo. Kufahamu  jinsi  unavyo  weza  kusaidia mtu wa  ugonjwa  wa  moyo  kuna bidhaa zake.

6.  Kupwaya  kwa  mishipa  ya  vena.

Kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  kwenye  uume   kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika  sehemu  nyingine  za  mwili.  
  
Mishipa  ya  vena  iliyopo  karibu  na  uume  kazi  yake  kubwa  ni  kuhakikisha  hakuna  damu  yoyote  kwenye  mishipa  ya  uume. ( KUMBUKA  KUWA  DAMU  NDIO  HUFANYA  UUMU  USIMAME, HIVYO  CHOCHOTE  KILE  KITAKACHO  FANYA  DAMU  ISIKAE  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME , KITAFANYA  UUME  USINYAE  )

Ili  uume  uendelee  kusimama  ni  lazima, mishipa  ya  vena  isiwe  na  uwezo  wa  kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume  kupeleka  nje  ya  mishipa  ya  uume.

Na  ili  mishipa  ya  vena  isiwe  na  uwezo  wa    kunyonya  damu  kutoka  kwenye   mishipa  ya  uume  ulio  simama  na  kuipeleka  kwenye  sehemu  nyingine  za  mwili,  ni  lazima  mishipa  ya  uume  iwe  imara  na  thabiti  isiyo  na  hitilafu  yoyote  ile.

Mishipa  ya  vena  ikipwaya, mwanaume  hutokuwa  na  uwezo  wa  kusimamisha  uume  wako, na  ikitokea  umefanikiwa  kuusimamisha  basi  utasimama  ukiwa  legelege  sana  na  utasinyaa  ndani  ya  muda  mfupi  sana, kwa  sababu  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  uume  wako  na  kuufanya  usimame, itanyonywa  ndani  ya  muda  mfupi  sana  na  kutolewa  nje  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  wako  usimame.

Tatizo  la  kupwaya  kwa  mishipa  ya  vena  linasababishwa  na  kupiga  punyeto  kwa  muda  mrefu  pamoja  na  ugonjwa  wa  kisukari.

Kupiga Punyeto kwa Muda Mrefu:   Kupiga  punyeto  kwa  muda  mrefu  ni  moja  kati  ya  vyanzo  vikuu  vya  tatizo  la  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  Asilimia  kubwa  ya  vijana  wenye  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, linasababishwa  na  upigaji  wa  punyeto  kwa  muda  mrefu.

*Jinsi  Punyeto inavyosababisha  Ukosefu  wa  Nguvu  za  Kiume*

Unapopiga  punyeto  unakuwa  unaiminya  mishipa  ya  uume   ambayo  ndio  inaufanya  uume  usimame.
Matokeo  yake  unaifanya  mishipa  hiyo  ilegee na  kutokuwa  na  uwezo  wa  kusimama  tena.

Mishipa  ya  uume  iliyo  legea  kutokana  na  upigaji  punyeto, huleta  madhara  yafuatayo  :

i.  Huondoa  uwezo  wa  mishipa  ya  uume  kurelax.

( Unapopata  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, mishipa  ya  uume  ina relax  , mishipa  iki  relax  husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  kuruhusu  damu  kingie  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hatimaye  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  mgumu)

ii.Mishipa   ya  kiume  ikishindwa  ku relax  husababisha  mishipa  ya  ateri  kuziba

iii.Mishipa  ya  ateri  ikiziba, damu  haiwezi  kutiririka  kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume, na  hata  ikitokea  damu  imeingia  ndani  ya  mishipa  ya  uume  basi  huingia  kiasi  kidogo sana   tena  kwa  presha  ndogo  sana  hivyo  basi  hata  kama  uume  utasimama   basi  utasimama  ukiwa  legelege  sana.

iv. Mishipa  ya  uume  ikishindwa  kurelax  basi  haitakuwa  na  uwezo  wa  kuipush  na  kuiziba  mishipa  ya  vena  ambayo  ndio  hunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume  ulio  simama. 
  
Matokeo  yake  basi, damu  kidogo  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuufanya  uume  kusimama, hunyonywa  na  kutolewa  nje  ya  mishipa  ya  uume  ndani  ya  sekunde  chache  sana  na  hivyo  kuufanya  uume usinyae  ndani  ya  muda  mfupi  sana.

v. Mishipa  ya  uume  kulegea

vi. Uume  kurudi ndani  na  kusinyaa  na  kuwa  kama  uume  wa  mtoto

6.  Tatizo  la  unene  kupita  kiasi : 
Tatizo  la  unene  na  uzito  kupita  kiasi  ni  miongoni  mwa  mambo  yanayo  sababisha  upungufu  wa  nguvu  za  kiume. 
  
Unene  kupita  kiasi  humuweka  mtu  katika  hatari  ya  kupatwa  na  magonjwa  kama  vile  kisukari, presha, moyo  na  shinikizo  kuu  la  damu.
  
 Na  magonjwa  ya  kisukari, moyo,presha  na  shinikizo  la  damu  husababisha  upungufu na  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, na  hivyo  kumuweka  muhusika  katika  hatari  kuu  ya  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Hivyo  basi  kwa  wewe  mwenye  tatizo  la  unene  na  uzito  kupita  kiasi , pamoja  na  kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume,  ni  vyema  ukafanya  na  mpango  wa  kupunguza  unene  na  uzito  wako.

(Jinsi  ya  kupunguza  Uzito tuna bidhaa za kupunguza uzito kama C9 na FIT 1&2)

7.   Matatizo  Katika  mfumo  wa  Ubongo

Uume  hauwezi  kusimama   bila  ya  kuwa  na  ushirikiano  na  ubongo.  Ili mtu  uume  uweze  kusimama, mtu  lazima  apate  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa  (UBONGO  UNA HUSIKA  HAPO ), akishapata  wazo, ubungo  hupeleka  ishara  kwenye  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo hupeleka  taarifa  kwenye  mishipa  ya  uume  then  uume  usimama.  
  
 Hivyo  basi  ili  mtu  aweze  kuwa  na uwezo  wa kusimamisha  uume  wake  ni lazima  kuwa  na  mawasiliano  mazuri  na  imara  kati  ya mishipa  ya  fahamu ( ubongo ), mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo   na  mishipa  ya  kwenye    uume.  Bila  ushirikiano  kati  ya  vitu  hivyo  vitatu, uume  hauwezi  kusimama.

Magonjwa  yanayoweza  kuathiri  ushirikiano  kati  ya  mishipa  ya  ubongo  na  mishipa  ya  uume, yanaweza  kusababisha  kushindwa  kusimama  kwa  uume.

Magonjwa  hayo  ni  pamoja  na  kiharusi,kupoteza  kumbukumbu  (  Alzheimer ), multiple  sclerosis pamoja  na  ugonjwa  wa  Parkinson.

Ni  vyema  mgonjwa  akatibiwa  kwanza  magonjwa  hayo  kabla  ya  kuanza  kutumia  dawa  ya  nguvu  za  kiume.  Kufahamu  jinsi  ya  kujitibu  magonjwa  tajwa  hapo  juu  kwa  njia  asilia,tafadhali  tembelea

Mambo   mengine  yanayo  sababisha  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  pamoja  na  maumivu & majeraha  kwenye  uti  wa  mgongo,  chango  la  kiume , ngiri  na  matatizo  katika  homoni.
[17/07/2016 23:05] Andrew: *V.* *MTU MWENYE SHIDA YA NGUVU ZA KIUME ATAJUAJE? AU WEWE UTAJUAJE NI I CA KUMUULIZA MTEJA WAKOMA ILI KUJUA KAMA ANA SHIDA HIYO? SI LAZIMA UMUULIZE ILA UNAWEZA KUMUELEZEA TU AKAJIKUTA YEYE MWENYEWE ANAKWAMBIA*

Zingatia usiri mkubwa mno. Licha ya kwamba sisi siyo madaktari lakini ni vema kutunza siri za mteja wako hasa kwenye changamoto za aina hii.

Tuendelee...

*Mtu Mwenye Shida ya Nguvu Za Kiume Atajuaje?*

Vifuatavyo ni viashiria  vya  mtu  mwenye  tatizo  la  Ukosefu/Upungufu  wa  Nguvu  za  Kiume.

Mtu  mwenye  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  huwa  na  dalili  zifuatazo:

1. Kushindwa  kabisa  kusimamisha  uume  wake

2. Uume  kusimama  ukiwa  legelege

3. Kuwahi  kumaliza  tendo  la  ndoa

4. Mwanaume  kutokuwa  na uwezo  wa  kufanya  tendo  la  ndoa  katika  baadhi  ya  staili  ( Mara  nyingi   mwanaume  huyu huwa  na  uwezo  wa  kufanya  tendo  la  ndoa    staili  moja  tu ).  Hapa  mwanaume  anakuwa  na  uwezo  wa  kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  staili  ya   “ missionary” pekee.  Ikibadilishwa   staili, mwanaume  anakuwa hana  tena  uwezo  wa  kusimamisha  uume  wake . japo  katika  hali  ya  u lege  lege

5. Uume  kutokuwa  na  uwezo  wa  kusimama  wenyewe   bila  kushikwashikwa  ama  kutomaswa kwa  muda  mrefu.

6. Uume  kusinyaa  ukiwa  ndani  ya  mwanamke.

7. Uume  kusinyaa, pindi  inapotokea  activity  yoyote  ya  kiungo  ama  ogani  nyingine  ya  mwanaume  wakati  wa  tendo  la  ndoa. Kwa  mfano, wakati  wa  tendo  la  ndoa, ikitokea  mwanaume  amekohoa  au  kupiga  chafya, uume  nao  unasinyaa.

8. Uume  kusinyaa  mara  tu  baada  ya kutolewa  ndani  ya  uke ( Kwa  mfano  kama  unafanya  tendo  la  ndoa, halafu  uume  ukatoka  nje, kitendo  cha  kuushika  kuurudisha ndani, tayari  una  sinyaa )

9. Kutokuwa  na  uwezo  wa  kurudia  tendo  la  ndoa.

10.  Kupatwa  na  maumivu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

*Mwanaume Asiye na tatizo la Nguvu Za Kiume Anakuwaje?*

Viashiria  vya  mwanaume  asiye  na  tatizo  la  Ukosefu  wa  nguvu  za  kiume

Mwanaume  asiye  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, huonyesha  ishara  zifuatazo:

i. Uume  husimama  ukiwa  imara  kama  msumari.

ii.Hukaa  kifuani  kwa  muda  mrefu  ( Wastani  ni  kati  ya  dakika  20  hadi  45  )

iii. Huweza  kurudia  tendo  la  ndoa  zaidi  ya  mara  tatu  bila  misuli  ya  uume  kuchoka.

iv. Huweza  kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  staili  yoyote  ile.

v. Uume  husimama  wenyewe  bila  kushikwa  shikwa  wala  kuwa  stimulated  kwa  namna  yoyote  ile.

vi. Kwa  ufupi  anakuwa  na  uwezo  wa  kufanya na  kukamilisha  tendo  la  ndoa  kwa  uukamilifu  mkubwa.

HIVYO,zifuatazo ni bidhaa zetu ambazo zinaweza kumsaidia mtu mwenye tatizo hilo,ikumbukwe bidhaa hizi sio dawa bali ni chakula cha nyongeza(supplements )

Tuwasiliane 0673214813…………whatsApp
josinah.jl@gmail.com

HISTORIA YANGU.

TIMIZA NDOTO ZAKO.

habari……………

naitwa Josinah Leonard Nzilayilunde,ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma(UDOM ) nikiwa nasoma shahada ya kwanza ya saikolojia ya watu wenye mahitaji maalumu(BA of education in special needs  ).

Kifamilia mimi ni mtoto wa kwanza ktk familia ya watoto wawili,familia yetu tunaishi na mama.Nikiwa kama binti mwenye kujipenda nilitamani sana kuwa na maisha mazuri,lakini kutokana na hali ya nyumbani kua ya kawaida nilijikuta ninavyo tamani haviendani na maisha yetu.Mara nyingi sana nilitamani kua na nguo nzuri zaidi,viatu,mikoba ya bei,gari la kutembelea na nyumba nzuri ya kuishi.lakini pia nilikua napenda kusaidia wahitaji ktk jamii yetu.

Nilianza biashara ndogo ndogo za kuuza nguo za mitumba,kuuza samaki,mihogo(vitafunwa ) na nilianza kucheza michezo ya upatu lengo ilikua ni kufikia ndoto zangu,lakini sikufika mbali kwani nilipata hasara sana.Muda huo nikihangaika hivyo nilikua nimemaliza kidato cha 4,hivyo matokeo ya kwenda kidato cha 6 yalikua mazuri hivyo nilianza masomo August 2013.

Nikiwa shuleni,nilijikuta natamani tena maisha ya wenzangu kwani walikua wanapewa pesa za kujikimu kwa upande wangu pesa ilikua chache hivyo sikua na ujanja zaidi ya kutulia tu,nikiwa bado shuleni nilianza biashara ya kuuza pipi na nguo za ndani za wadada pia urembo.Lakini bado sikufanikiwa.Hivyo nilimaliza kidato cha sita 2015,May

Baada ya kurudi nyumbani mambo yalizidi kua magumu kwani sikua na uwezo wa kumudu biashara yoyote kutokana na kukosa mtaji.Hivyo nilienda kukopa pesa kwa rafiki yangu nikaanza kuuza mihogo ya kukaanga,pia kupika uji.Hali hii iliniumiza sana kwani nilitumia muda mwingi sana bila faida niliyo itaka.Hivyo nilitamani hata kupata mwanaume wa kunihudumia.Haikua vizuri mimi kufanya hivyo japo sikuweza kupata mwanaume huyo hivyo nilipiga moyo konde na kuendelea na biashara zangu.kwasababu wanawake wengi wanapo shindwa kufanya shughuli zao wanakimbilia kutafuta wanaume.

Mnamo September 11 nilikutana na habari nzuri huko Facebook iliyokua inahusu fursa ya biashara ya mtandao(network marketing ) nilivutiwa sana na mfumo huo wa biashara,na sikusita kuanza biashara hiyo kupitia kampuni ya forever living.Kwa muda wa miezi 4 nilijipanga kupata mtaji kisha nikaanza biashara rasmi January 11 ya mwaka 2016.naweza kusema huu mwaka ni wa HABARI NJEMA.kwasababu fursa hii ya biashara imenipa mtazamo mpya.

1.Nimenufaika sana na afya,kwa kutumia bidhaa zenye ubora.mimi na familia yangu tumenufaika na afya.hatusumbuliwi tena na magonjwa kwani afya zetu ziko imara.


 2.Kupitia biashara hii nimejifunza kuwapenda watu walio fanikiwa ninawachukulia mfano ktk maisha yangu na safari ya mafanikio,hapo nyuma sikuwapenda matajiri kwasababu niliaminishwa kwamba wao wanakandamiza masikini kumbe sivyo,kupitia biashara hii nimejikuta napenda sana kujifunza kwa matajiri walio fanikiwa kwasababu wao pia walianza kama sisi,isipokua wao walibadili mtazamo na kujifananisha na washindi na hawakukata tamaa kufikia ndoto zao hata walipoanguka walisimama kuendelea na safari ya mamafanikio.kwangu mimi hii ni hatua kubwa sana.


3.Kupitia biashara hii nimejifunza uvumilivu kua na msimamo kwa ndoto zangu,naamini nitapata mafanikio makubwa kwasababu bado naendelea kujifunza lakini pia bado naendelea kuwaongoza wenzangu nao wafikie ndoto zao,naamini wenzangu wanapo fanikiwa kutokana na muongozo wangu ndipo hapo na Mimi nafanikiwa.hapo mwanzo nilifikiri kufanikiwa peke yangu tu kumbe sikua sahihi hivyo kupitia biashara hii nimejifunza upendo.

4.Kupitia biashara hii nimejifunza namna ya kutumia pesa,hapo nyuma nilikua nikitumia pesa bila mpangilio,sasa hivi ninaelewa maana ya akiba na kukuza uwekezaji kutokana na akiba ili niwe na mzungumko mzuri wa pesa,pia nimeamini kwamba ppesa inaweza kumtumikia mtu yoyote endapo tu utakua tayari kubadili mtazamo 

5.Kipato,fursa hii imenisaidia kutengeneza kipato kizuri,kupitia kipato ninacho pata sasa nimeanza kuamini kua mtu yoyote anaweza kufikia ndoto zake,kwa mwezi nimeweza kujikimu mahitaji madogo madogo kama binti lakini pia nimeweza kusaidia familia yetu kuweza kujenga nyumba ya kuishi,hivyo tumetoka ktk mazingira ya kupanga.lakini pia kipato hicho kinaongezeka siku hadi siku tofauti na ajira kwasababu mara nyingi mishahara haikutani,pia mshahara haupandi kwa walio chini.Hivyo naamini kupitia biashara hii ninakua milionea ndani ya miaka 5 tu.

6.kupitia biashara hii nimepata muongozo kwa wenzangu walio nitangulia ktk biashara hii kwa mafunzo mbalimbali,hii imeniondolea woga wa kuthubutu kwasababu nimeshikwa mkono.tofauti na biashara nyingine nimeona huku kuna umoja sana sana.Hivyo naona ni mahali salama kwangu na kwa mtu yoyote kutimiza ndoto zake.


7.Nimeweza kuwaongoza ndugu jamaa na marafiki kuweza kufanya biashara hii kwani ktk biashara hii tunasaidiana ili kila mtu kufikia malengo yake,hii ilikua ndoto yangu ya miaka mingi kusaidia watu kwa namna mbalimbali hivyo kupitia fursa hii naendelea kugusa maisha ya wengi,hivyo hata wewe unae soma ujumbe huu unaweza kwasababu tutakushika mkono.

8.Nimejifunza mambo mengi ambayo sikufundishwa shuleni,hasa swala la kutunza muda,kutunza pesa,kuwa kiongozi,kuongea na watu,nimepata mtazamo mpya juu ya mafanikio kwani hapo awali nilifikiri haiwezekani mimi kufanikiwa lakini kupitia fursa hii nimebadili sana mtazamo wangu juu ya mafanikio sasa ninaamini ktk mafanikio.

9.Kupitia biashara hii nimeweza kusafiri na naendelea kusafiri dunia,kwani kampuni yetu inatupa nafasi ya kusafiri angalau mara mbili kila mwaka kwenye nchi mbili tofauti.Hivyo safari hizi zinanijengea kujiamini pia kujifunza zaidi.

10.kupitia biashara nimejifunza mafanikio sio kwa wasomi tu,bali ni kwa kila mtu hata ambao hawajasoma kwasababu kitu cha kwanza kinacho onesha kua unahitaji mafanikio ni jinsi akili yako inavyo kubali,pia juhudi kwasababu nimeona wasomi wengi lakini bado maisha yao ni magumu,hivyo biashara hii imeniondolea matabaka ktk mafanikio,kufanikiwa ni kuiandaa kwanza akili kisha kuambatana na walio fanikiwa,kua tayari kusaidia hakika utajifunza mengi ambayo huwezi kuyapata darasani.

11.kupitia biashara hii nimeweza kupata marafiki wapya wenye mitazamo chanya ambao wananiongoza ktk hatua za mafanikio.Naamini nguvu ya marafiki wenye mtazamo chanya ktk safari ya mafanikio kwasababu marafiki walionizunguka ndio wanao tafsiri muonekano na mtazamo wangu,hivyo hii biashara kwangu imekuwa zaidi ya maisha.nimejifunza kumbe marafiki wanaweza kuchangia kufanikiwa kwangu hivyo naendelea kutazama marafiki wengi zaidi wenye mitazamo chanya ili niendelee kujifunza kutoka kwao.hata kwako wewe inawezekana angalia sana marafiki walio kuzunguka.

Hizo ni baadhi ya faida nilizo pata kutokana na biashara hii ya mtandao kupitia kampuni ya forever living.hivyo kwa kumalizia napenda kukutia moyo unaesoma story yangu amini kua inawezekana kubadili maisha yako hivyo kama unazo ndoto usisite kuzitimiza.

KUTANA NA FOREVER LIVING,IKUBADILISHE MAISHA YAKO.

JOSINAH LEONARD NZILAYILUNDE.

#0673214813……………WhatsApp

josinah.jl@gmail.com

ELIMU YA NGUVU ZA KIUME.

IJUE Arg+

#ARGI+ Hii ni bidhaa asili na maalumu sana kwa afya ya Yeyote yule. Ni bidhaa ambayo ilishinda tuzo ya Nobel Duniani kwa wanaofuatilia tuzo hizo kutokana na Ubora wake. Ni bidhaa yenye faida nyingi sana kwa mwili wa Binadamu...
1.Inakiondosha sumu muhimu sana Mwilini.
2.Inazalisha #Anti-aging hormone na kutengeneza seli mpya za damu hivyo kuzuia kuzeeka kwa kasi.
3. Inaondoa #Cholestrol yaani Mafuta Machafu Mwilini.
4.Inasababisha Mzunguko wa Damu kwenda vizuri yaani damu kufika kila mahali vizuri hivyo kusaidia #Nguvu_za_kiume kwa wanaume kuwa sio tatizo.
5. Inaondoa Maumivu makali ya Viungo hasa kwa #Wanawake_wanaosumbuliwa_na_maumivu_ya_kiuno_na_mgogo.
6.Inapambana sana na #Pressure kwani Inapelekea mzunguko wa damu kukaa sawa.
7. Inabalance Sukari Mwilini hivyo husaidia sana kwa Mwenye #Kisukari.
8.Kwa wanamazoezi ni nzuri kwani husaidia kujengeka mifupa na misuli pia kupata nguvu.
9.Inaboresha Muonekano wa #Ngozi kutokana na uwezo wakuzalisha seli mpya kwa wingi.