Jumatatu, 5 Septemba 2016

TAMBUA MAKUNDI YA WATAFUTA PESA.

.

JE, UPO KUNDI GANI KATI YA HAYA?

Kuna makundi manne (4) ya watu wanaotengeneza pesa hapa duniani.

1. WAAJIRIWA.
Hawa ni watu ambao kimsingi wanauza muda wao almost wote wa siku nzima kwa mwajiri wao na yeye anawalipa pesa kwa kuwaambia cha kumfanyia. Kwa kuwa kanuni ya mshahara huwa ni kumlipa mtu 10% ya anachozalisha hasa kwa makampuni makubwa basi haitakaa itokee mwajiriwa kulingana kipato na mwajiri wake. Na hivyo wengi wa waajiriwa hufa #maskini na watoto wao pia kuanza kutafuta maisha kivyaovyao kwa kusoma na kuja #kuajiriwa pia hivyo hivyo..
Usikubali kubaki kwenye ajira unalipwa laki 5 kwa mwezi sawa na Tsh 1,850 yaani chini ya dola moja kwa saa. Ina maana umesoma mpaka chuo kikuu halafu thamani ya lisaa lako moja ni less than $1!!!!? Ndiyo maana watu wengi waliosoma sana huwa hawawezi kuwa matajiri kwa sababu wanauza muda wao kwa "bei chee" halafu siku zinazidi kuyoyoma haoni mafanikio. Huku tena ana mkopo wa gari nk. Makato na marejesho... Kwa nini usife masikini kwa style hiyo.?

2. WALIOJIAJIRI
Hawa hujitambua kidogo na kuamua kufanya kazi binafsi au kufungua biashara ndogo kama duka nk. Lakini kwa kuwa hawana pesa ya kununua muda wa watu wengine na kuwaajiri hawa nao huwa busy kutwa kucha bila mafanikio ya maana. Ana duka miaka 15 sasa halijawahi kupanuka likawa supermarket. Na mara nyingi huyu mtu akifa na biashara yake nayo humfuata. Ndo watu wanasingizia eti alikuwa na biashara za "uchawi". Kumbe shida ni kuwa kila kitu kilikuwa kinamtegemea yeye.

3. WAMILIKI WA BIASHARA KUBWA
Hawa huwa na kipato endelevu (residual income) maana amemunua muda wa watu weeengi kawaajiri halafu kawapa majukumu kwa hiyo awepo asiwepo pesa inaendelea kuingia kwake. Mfano kina Bakhressa, Mengi, Dewji, etc. Majina yao yanajulikana. Ni wachache nchi hii. Ukihesabu vidole vyako vya mikono na miguu majina yataisha kabla hujamaliza kuhesabu.

4. WAWEKEZAJI
Hawa ni watu wenye pesa nyingi zaidi na wana uwezo wa kuiwekeza mahali hata nje ya nchi ikawa inawazalishia pesa zaidi bila wao kuwepo kabisa. Hawa hata majina huwa  hawajulikani

Kwa hiyo nadhani tayari wewe unajua kundi lipi upo (ama kama wewe ni mwanafunzi unaweza kuona kundi lipi unaelekea).

SASA SIKIA...
Makundi mawili ya kwanza ni makundi ya watu maskini. Mfano waajiriwa ni watu wanaotumia muda wao na nguvu na maarifa yao yote (waliyoyakusanya kwa miaka mingi ya kusoma kwa shidashida) kumtajirisha mtu kwa malipo kidogo yanayomwezesha huyu muajiriwa kulipa kodi (siyo kujenga), kula, kuvaa,  kusafiri kwenda na kurudi kazini nk. Yaani basic needs tu. Maisha ya waajiriwa wengi yanafanana. Mfano ni wachache sana katika ajira ambao wamejenga nyumba zao binafsi kwa hela halali ya ajira. Kama vile ilivyo vigumu kwa mwanafunzi kwenda chuo kwa gari lake mwenyewe alilonunua kwa pesa yake halali. Wapo wachache sana. Na hivyohivyo waajiriwa kumiliki nyumba. Wengi wamepanga. Jiulize lini utafikia hizi level especially kama utang'ang'ania ajira tu bila kujishughulisha na kitu kingine cha ziada mpaka uzeeni? Ndo unastaafu unapewa kiinua mgongo lakini miaka 7 tu baada ya hapo unakufa kwa pressure. Coz ndo unaanza kuona wengine wa umri sawa na wewe wako mbaaaali kimaisha hapo nguvu za kuhimili mikikimikiki ya biashara huna tena watoto na wajukuu hawana future unaanza kupata stress. Kisa ulikuwa ungependa kiyoyozi cha kazini. Haya, endelea kufurahia kiyoyozi ndugu. Halafu mi huwa nashangaa..yaani unajua kabisa hapo kazini kuanzia kiti, dawati, computer, kalamu, karatasi, kula kitu si cha kwako. You are just hired to use them to produce for someone else. Hebu tufunguane macho leo..

Waliojiajiri nao wako busy. Kama ana duka basi kufata mzigo yeye (hamwamini mtu), kuuza yeye, usafi yeye, kuhesabu stock yeye, ulinzi wa duka yeye ndo analinda maana analala humo humo. Kama jongoo alivyo na miguu mingi lakini spidi "kiduchu" ndivyo na huyu nae. Miguu mingi ya jongoo bila macho is equal to ZERO. Na hivyo hivyo shughuli nyingi bila maarifa is uqual to ZERO. Yaani yuko busy kila saa lakini spidi ya mafanikio ni ndogo kweli kweli. Sasa maendeleo hayaji kwa style hiyo ila kwa kuwa hajui anahisi siku moja na yeye atakuwa kama Bakhressa. Kwani Bakhressa ndo anauza ice cream za Azam? Hujiulizi?

KWA WANAFUNZI..
Bahati mbaya sana kama ni mwanafunzi uko sekondari au chuo hiyo ndo ramani ya future yako. Ukimaliza chuo lazima uingie katika makundi hayo mawili ya kimaskini hasa kundi la kwanza. Na siku hizi ajira wala usitegemee. Utafiti unaonyesha kuwa katika watu 1,200,000 wanaohitimu vyuo mbali mbali kila mwaka ni 200,000 tu wanaobahatika kupata ajira.  Hao milioni moja za zaidi wanakaa huku mtaani bila ajira.  Fikiria sasa itakuwaje.

HATA HIVYO.. kuna njia ya kukusaidia kuweza kuhama kutoka makundi hayo mawili kwanza na kuingia makundi mawili ya mwisho hapo juu.
Cha msingi ni Wewe kujishusha tu na kukubali  kuwa unahitaji kujifunza hivi vitu. Lakini ukifikiri kuwa unajua kila kitu kuna maarifa utayakosa simply kwa kutothamini mawazo ya wengine ambao huenda ni Mungu tu anawaleta ili kukustua kidogo upate ufahamu fulani lakini wewe aaah. Umeziba maskio na pamba umeweka. Uko busy. Uko determined kufa maskini. Hebu jifunze. Itakusaidia. Kama umeajiriwa na unasoma ujumbe huu hebu jiulize ajira yako ikiisha leo ghafla PAAP!! Utaanzia wapi? Kama utaandika CV tena basi kubaliana na hali halisi tu kuwa wewe ni maskini. Huna cha kuuza kupata pesa zaidi ya muda wako. Kumbuka rasilimali ambayo Mungu aliwagawia wanadamu wote sawa ni MUDA. 24 hours kwa kila binadamu. Matajiri wananunua muda wewe unauuza. Yaani unafanya opposite na wanachofanya matajiri halafu unasema unataka kuwa kama wao. Unanielewa? Kuna mtu maarufu duniani anaitwa William Gates III au kwa jina maarufu Bill Gates, anasema, "KAMA ULIZALIWA MASKINI HILO SIYO KOSA LAKO ILA UKIFA MASKINI HILO NI KOSA LAKO". Jifunze.

Kuna tajiri mwingine anaitwa JACK MA huyu ni mmiliki wa ALIBABA. Yeye anasema hatua kuja duniani kufanya kazi tu mpaka siku ya kuta bali tulikuja kuishi maisha yetu. Anasema kuifanya kazi tu mpaka mwisho wa maisha yako utakuwa hujawahi kuishi maisha yako. Anasema siri ya mafanikio ni kutafuta kazi ambayo utaifanya kwa miaka mitano Kisha iwe imekupa pesa za kuishi maisha yako. Tafuta mpaka upiate. Kama hujaipata tafuta tu. Kama bado hujaipata watafute waliokwishaipata.

Unaona mawazo hayo? Man,  I love that.  So..
Usikae tu unaenda kazini tu kila siku mwisho itakuwaje?

Na kama wewe ni mwanafunzi hii ni habari njema sana maana ukiamua kujifunza vitu hivi sasa hivi ukavifanyia kazi, then I assure you miaka miwili au mitatu mbeleni wakati wenzako wanasambaza CV kuomba ridhaa ya kuingia kundi la kwanza la umaskini wewe utakuwa unanunua gari lako la pili au hata kiwanja na huenda umeanza kujenga kulingana tu na ndoto zako ni zipi.

Waingereza wanasema LIFE BEGINS AT 40. Yaani maisha huanza ukiwa na miaka 40. Kwa maana kwamba ukiwa na umri huo hutakiwi kuwa unawaza ada za watoto zinatakiwa ziwepo ulishatafutaga siku nyingi ukiwa na miaka 20-39. Wakati ukifika miaka 40 unapaswa uwe na nyumba gari urithi kwa familia yako biashara zilizosimama nk. Siyo ndo unaandika CV kuomba kazi ya tatu ili kuongeza kipato.
Life begins at 40.
How old are you?

So....
Kama unaona huu ujumbe unakuhusu na umekugusa kwa namna moja au nyingine basi wasiliana nasi kwa WatsApp ................0673214813………
.. tukupe mpango madhubuti wa kubadili maisha yako!

Ijumaa, 5 Agosti 2016

*JINSI YA KUTUMIA MUDA VIZURI KWA AJILI YA MAFANIKIO YAKO YA KESHO*

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutumia Muda Wako Vizuri Na Kukuletea Mafanikio Makubwa.
Muda ni ma li! Huu ni usemi maarufu sana kwa vijana na wazee. Unaonekana ni usemi wa kawaida na uliozoeleka kwa watu wengi, maskini na matajiri, wanawake na wanaume. Japokuwa watu wengi tunautumia usemi huu, lakini baadhi yetu hatuelewi maana yake na wengi wetu hatuutumii katika maisha yetu.
Muda ni mali maana yake kila kitu, vitu vyote vinavyoonekana vidogo na vikubwa ni matokeo ya matumizi ya muda. Hata mimi na wewe ni matokeo ya matumizi mazuri ya muda. Kila mafanikio yaliyowahi kutokea na yanayoendelea kutokea ni matokeo ya matumizi mazuri ya muda. Kwa hiyo kuna uhusiano mkubwa sana kati ya mafanikio na matumizi ya muda,yaani muda ukitumika vizuri mafanikio yanapatikana na muda huo huo usipotumika vizuri hakuna mafanikio.
Hakuna haja ya kueleza na kufafanua maana ya muda, ila nataka ujue kuwa kuna aina za muda, ndiyo zipo aina mbili za muda. Aina ya kwanza ya muda ni MUDA WA SAA. Muda huu unaanzia sekunde hadi mwaka. Katika muda wa saa, tunaposema miaka miwili ni miaka miwili, haizidi wala haipungui.Tunaposema huyu ana miaka hamsini ina maana mtu ameishi vipindi hamsini ambapo kila kipindi kina jumla ya miezi kumi na mbili, haizidi wala haipungui.
Aina ya aili ya muda ni MUDA HALISI. Muda halisi unaundwa na muda wa saa na matukio. Katika aina hii ya muda tunaangalia matukio yaliyotokea katika muda wa saa husika.Tunalinganisha idadi ya miaka na miezi na matukio au mafanikio yaliyopatikana katika kipindi husika. Watu wanaweza kuwa sawa katika muda wa saa lakini wakawa tofauti katika muda halisi. Mtu anaweza kuwa na umri wa miaka sitini(katika muda wa saa) lakini akawa kwa mafanikio ni kama mtu aliyeishi miaka thelathini tu.
Na pia mtu mwingine anaweza kuwa na umri wa miaka thelathini, lakini akawa na mafanikio makubwa sana kimaisha kama mtu aliyeishi miaka mingi sana duniani, yawezekana hata miaka sabini. Usichanganyikiwe, nalinganisha muda wa saa na mafanikio. Muda halisi unatuambia kwamba kuna kuchelewa katika maisha. Muda halisi unatukumbusha kuwa kuna wakati tunaweza kupoteza miaka yetu bila kujua. Unatukumbusha kufanya jambo sahihi kwa wakati sahihi.
Tumejifunza aina za muda na tofauti zake, sasa tuangalie matumizi ya muda wa saa.Tunatumia muda huu kufanya mambo matatu ambayo yanatuleta kwenye muda halisi, tukiwa tumewahi au tumechelewa tunatumia muda katika
kufikiri, kusema au kuzungumza na kufanya mambo mbalimbali katika maisha yetu.
Baada ya kuangalia matumizi ya muda wa saa, tumegundua kuwa tunautumia muda kama chombo kutusafirisha kutoka katika ulimwengu wa namba na mahesabu kwenda kwenye ulimwengu wa halisi,ulimwengu wa vitendo ambapo tunaweza kufanya tathmini na kuona kuwa tumewahi au tumechelewa, tuko nyuma au tuko mahali sahihi.
Sasa tuangalie mambo ya kufanya ili tuweze kuutumia muda wa saa na kufikia mafanikio ambayo yataweka uwiano sawa kati ya muda wa saa na muda halisi katika maisha yetu.Yapo mambo mengi ambayo unapaswa kuyafanya ili uweze kutumia muda wako vizuri, baadhi ya  mambo hayo ni haya yafuatayo:-
1. Weka kumbukumbu ya mambo unayofikiria, unayoyasema na kutenda.
Kumbukumbu ni muhimu sana katika maisha ya binadamu kwa sababu ndizo zinazotusaidia kufanya tathmini. Jitahidi kuweka kumbukumbu za mambo unayofikiri, unayosema na kutenda japo kwa siku moja. Mwisho wa siku jitahidi kukukumbuka mambo uliyofikiria, uliyosema na kutenda yawe mazuri au Mabaya. Hii itakusaidia kufanya tathmini ya matumizi ya muda kwa siku hiyo.
Tathmini hiyo itakusaidia pia kujua umetumia muda vizuri au vibaya. Mara nyingi sana siyo rahisi kukukumbuka mambo yote uliyofikiria na kusema lakini ni rahisi kukukumbuka matukio na mara nyingi matukio hutokana na kufikiri na kusema,kwa hiyo kukumbuka matukio ni njia rahisi zaidi yakukuwezesha kufanya tathmini ya siku nzima.
2. Weka ratiba ya siku nzima.
Ratiba ni muhimu sana katika maisha ya kila siku.Usianze siku bila kujua utafanya nini siku hiyo. Unaweza kuweka na kupanga ratiba ya siku inayofuata kabla ya kulala au asubuhi kabla hujaanza jambo lolote. Watu wote waliofanikiwa, wamefanikiwa kwa sababu ya matumizi mazuri ya muda, wanafanya kazi zao kwa ratiba na wana nidhamu linapokuja swala la matumizi ya muda. Bila kuwa na ratiba muda hutumika bila mpangilio na wakati mwingine muda hupotea bure. Unapoweka ratiba hakikisha kila kitu ulichokiweka kina wakati na muda wake. Kinaanza saa ngapi na kuisha saa ngapi. Ni vyema ratiba hii iwe na mambo ya msingi tu. Usisahau mapumziko. Mapumziko ni muhimu kwa utendajibora wa akili na mwili.
3. Epuka kuwa na mipango mingi.
Katika ratiba yako usiweke mambo mengi sana ambayo utekelezaji wake ni mgumu au yanachosha.Weka mambo machache ambayo yanakupa nafasi ya kupumzika na kutafakari namna ya kuianza siku inayofuata. Ukiweka mambo mengi kuna hatari ya kuyatekeleza nusunusu na mengine yanaweza yasitekelezwe kabisa.
4. Usiruhusu mambo yasiyo ya msingi kuingilia ratiba yako.
Mara unapoanza kutekeleza mipango ambayo iko kwenye ratiba yako, usiruhusu mambo yasiyo ya msingi kuingilia na kuvuruga ratiba yako. Kuwa na nidhamu na heshimu ratiba yako. Zipo dharura lakini si dharura zote zinahitaji kushughulikiwa papo .Kama dharura ni ya msingi na inahitaji kushughulikiwa papo hapo hamna tatizo.Jifunze kutambua na kutofautisha dharura zinazohitaji kushughulikiwa papo hapo na zile zinazoweza kushughulikiwa baada ya ratiba kukamilika.
Kuna watu ambao wako tayari kuvuruga ratiba zao na kuacha shughuli zao kwa sababu ya mambo yasiyo ya msingi kwa mfano kuangalia mechi na burudani zingine ambazo haziwasaidii katika maisha yao. Narudia tena,uwe na nidhamu heshimu ratiba yako.
5. Epuka kutumia muda mwingi kufanya mambo yasiyo ya lazima na yasiyo na faida.
Epuka kutumia muda mrefu kufanya mambo yasiyo ya msingi na yasiyo na faida kwa mfano kuchati kwenye mitandao ya kijamii, kuangalia mechi na burudani zingine wakati ambapo unatakiwa kufanya mambo ya msingi kwa ajili yako na jamii inayokuzunguka. Sina maana mitandao ya kijamii mibaya ila nasisitiza kuwa na kiasi na kuipa nafasi ndogo katika maisha ya kila siku. Kama utakuwa unawasiliana kwenye mtandao wa kijamii basi iwe kwa faida na si kupoteza muda .
Ninasema hivi kwa sababu hili limekuwa tatizo Kubwa sana kwa kizazi cha sasa hasa vijana, tena wanafunzi ambao wanatakiwa wasome kwa bidii wasipoteze muda hata kidogo. Muda wa kufanya mambo ya msingi utumike kufanya mambo ya msingi na mambo mengine yapewe nafasi ya pili au ya mwisho.
5. Tumia sehemu Kubwa ya muda wako kufanya mambo ya msingi.
Unashauriwa kutumia 75% hadi 80% ya muda wako kufanya mambo yenye tija kwako na kwa wanaokutegemea.Tumia sehemu Kubwa ya muda wako kufanya mambo yatakayokujenga na kukuimarisha kiakili,kijamii na kiuchumi. Fanya kazi za kukuingizia kipato, soma vitabu, magazeti, na majarida yatakayokuongezea maarifa na kupanua ufahamu wako.Ukiingia kwenye Internet soma vitu vinavyokujenga na siyo kufuatilia habari za watu maarufu huku hakuna cha maana unachopata.
Wengine wanaingia kwenye Internet kuangalia ili kuangalia picha za ngono na utupu. Watanzania wengi watu wazima ukiwauliza walisoma vitabu lini, hawakumbuki, wengine wanakwambia shule ya msingi na wengine sekondari, inasikitisha. Wengine hata wanaponunua simu, hawasomi vile vitabu vinavyoelekeza namna ya kutumia hiyo simu. Watu walio wengi sana kama ni kusoma wanapenda kusoma vitu ambavyo haviwasaidii sana katika maisha yao kama magazeti ya udaku.

Naomba niishie hapo kwa maelezo zaidi tuwasiliane #0673214813…………whatsApp

Alhamisi, 4 Agosti 2016

AFYA NA UREMBO

AFYA NA UREMBO.

muonekano wako unaongezwa haiba na tabasamu la midomo yako,Midomo mikavu haivutii si kwa wanaume au wanawake ni wakati wako kutumia bidhaa ALOE LIPS
Imetengenezwa kwa
~Aloe vera
~Asali
~Jojoba oil

Kwa faida zifuatazo.

~Kulainisha midomo mikavu na inayo chanika

~Kuondoa utando mweupe mdomoni

~Kuondoa weusi unaotanda midomoni

~Unaweza kuipaka kama mafuta usoni

~Unaweza kuipaka kwenye vidole kuondoa mpauko unaosababishwa na kutumia sabuni kali

~unaweza kuipaka unapo ng'atwa na wadudu (kuzuia uvimbe na miwasho )

~Unaweza kuipaka unapotokewa na harara.

Ni ALOE LIPS,yenye matumizi zaidi ya moja kwa kurudia urembo wako.

Kwa mahitaji yako tuwasiliane utaletewa popote ulipo.

………0673214813………WhatsApp

Jumatano, 3 Agosti 2016

SIRI ZA MAWASILIANO YANAYOFIKISHA UJUMBE

[19/06/2016 01:22] Violeth: Siri Za Kukuwezesha Kushawishi Mtu Yeyote Akubaliane Na Wewe....                                      
Mawasiliano ni moja ya misingi muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Na pia ni moja ya mahitaji muhimu kama tunataka kuweza kufikia mafanikio makubwa kwenye jambo lolote ambalo tunalifanya. Kumbuka ya kwamba chochote unachotaka kinatoka kwa watu wengine, hivyo jinsi unavyoweza kuwashawishi na wakakubaliana na wewe ndivyo itakuwezesha kupata unachotaka. Na ushawishi unaanzia kwenye mbinu bora za mawasiliano ambazo mtu anakuwa nazo.
Watu wengi wamekuwa wakiwasukuma wengine ili kupata kile wanachokitaka. Na wamekuwa wakifanya hivi kwa kubishana, kutisha, kudanganya na hata kulaghai ili wapate wanachotaka. Kwa njia hizi inakuwa vigumu zaidi kwa watu kuwa tayari kutoa kile ambacho wengine wanakitaka. Ni kutokana na changamoto hii Daktari na Mwanasaikolojia Mark Goulston alipokuja na kitabu ambacho kina mbinu bora za ushawishi ambazo zinamwezesha mtu kupata kile anachokitaka kutoka kwa mtu yeyote. Daktari Mark anatumia taaluma yake na uzoefu wake kwenye kazi ya ushauri katika kutushirikisha mambo haya muhimu ya kuzingatia kwenye mawasiliano yetu.
Karibu tujifunze kwa pamoja;
1. Kila mtu ana mahitaji yake, matamanio yake na pia ajenda zake. Kila mtu ana siri yake ambayo anaificha, ambayo hataki wengine waijue. Na pia kila mtu yupo bize, ana msongo wa mawazo, na hana muda wa kumtosha kufanya kila anachotaka kufanya. Ili kuweza kwenda na hayo yote yanayoendelea kwenye maisha yake, mtu anajitengenezea ukuta ambao bila ya kujua hayo huwezi kumshawishi kwa jambo lolote. Kabla hujataka mtu afanye au akupe chochote unachotaka, anza kwanza kuvunja ukuta huu ambao kila mtu amejijengea.
2. Ushawishi unaenda kwa mzunguko ambao una hatua tano muhimu. Yaani kabla mtu hajashawishika kufanya chochote unachomwambia, anapitia hatua hizi tano ambazo unatakiwa kuzijua na kujua jinsi ya kumpitisha mtu kwenye kila hatua;
Hatua ya kwanza ni kumtoa mtu kwenye kukataa mpaka kuwa tayari kusikiliza. Wakati wowote mtu yupo kwenye hali ya kukataa, unahitaji kuwa na mbinu ya kumfanya akusikilize.
Hatua ya pili ni kumtoa kwenye kusikiliza mpaka kukufikiria. Hapa mtu anakuwa amesikiliza kile ulichomwambia, na kuna mbinu bora za kumwambia na akaanza kufikiria kwamba anaweza kufanya au anaweza kuwa tayari.
Hatua ya tatu ni kumtoa kwenye kufikiria mpaka kuwa tayari kufanya. Baada ya mtu kufikiria kwamba anaweza kufanya anashawishika zaidi na kuwa tayari kufanya.
Hatua ya nne ni kumtoa kwenye kuwa tayari kufanya mpaka kufanya. Hapa ndipo mtu anapofanya kile ambacho unataka afanye au anakupa kile ambacho ulitaka akupe.
Hatua ya tano ni kumtoa kwenye kufanya mpaka kufurahia kufanya na kuendelea kufanya. Kufanya siyo mwisho wa mzunguko huu, bali mtu anahitaji kufurahia kwamba amefanya na kuendelea kufanya kadiri inavyohitajika.
Huu ndio mzunguko wa ushawishi ambao unatakiwa kuujua na jinsi ya kuutumia kwa watu mbalimbali. Utajifunza hayo kwenye kitabu hiki.
3. Ili uweze kuwa na ushawishi kwa wengine unahitaji kuujua vizuri ubongo wa binadamu. Ubongo wa binadamu umegawanyika kwenye sehemu kuu tatu ambazo zinatofautiana kwa miaka ambayo zimekuwepo.
Sehemu ya kwanza ni ubongo wa chini ambao una tabia kama za mjusi. Hii ni ile sehemu ya ubongo ambayo kazi yake kubwa ni kuhakikisha unaishi (kwa kiingereza survival). Ubongo huu kazi yake ni kuhakikisha umepata chakula na unaweza kujikinga na hatari. Ubongo huu huwa unachukua hatua haraka bila hata ya kufikiri kwa kina. Kwa mfano kama umewahi kuwa kwneye hatari kama kukimbizwa na mnyama kama mbwa utakua umeona unapata nguvu nyingi hata za kuruka ukuta ambao kwa kawaida huwezi kuuruka, hii ndiyo kazi ya ubongo huu. Kwa kiingereza wanasema FIGHT-OR-FRIGHT.
Sehemu ya pili ni ubongo wa kati, ambao una tabia za mnyama. Hii ni sehemu ya ubongo ambayo imebeba hisia zote za mtu. Hisia za upendo, furaha, huzuni, hasira, maombolezo, wivu na hata raha zipo kwenye sehemu hii ya ubongo. Sehemu hii ya ubongo ndiyo inatusukuma kufanya vitu vinavyotupa hisia nzuri na kutuepusha na vitu vinavyoleta hisia mbaya.
[19/06/2016 01:24] Violeth: Sehemu ya tatu ni ubongo wa juu ambao una tabia za utu. Huu ndio ubongo ambao unatutofautisha sisi binadamu na viumbe wengine wote. Huu ndiyo ubongo ambao unafikiri kwa kina kwenye kila jambo tunalofanya au linalotokea. Huu ndio ubongo ambao unatunza kumbukumbu. Ubongo huu unakusanya taarifa kutoka kwenye sehemu nyingine za ubongo na kufanya maamuzi sahihi.
4. kwa bahati mbaya sana, watu wengi wamekuwa wakifanya maamuzi kwa kuongozwa na ubongo wa chini na ubongo wa kati. Ni mara chache sana watu wanaweza kuutumia ubongo wa juu vizuri na kufanya maamuzi bora. Maamuzi mengi yanayofanywa na ubongo wa chini na wa kati ni maamuzi ambayo yana faida ya muda mfupi lakini kwa muda mrefu yana hasara kwao. Mfano ni mtu ambaye anabaka, hapa anauridhisha ubongo wa kati ambao utapata raha, lakini angetumia ubongo wa juu angeona siyo kitu sahihi kwake kufanya.
5. Ili uweze kumshawishi mtu yeyote, hakikisha unaongea naye akiwa kwenye ubongo wa juu. Kama mtu hayupo kwenye ubongo wa juu, hakuna kitu unachoweza kumwambia akakusikia na kukuelewa. Haijalishi utatumia mbinu bora kiasi gani, kama mtu hayupo kwenye ubongo wa juu, unapoteza muda wako.
Hii ndiyo maana ni vigumu sana kumshauri mtu ambaye ana hasira, au aa furaha au yupo katikati ya hisia kali za mapenzi. Kuweza kumshawishi mtu mtoe kwanza kwenye ubongo wa kati na wa chini na mpeleke kwenye ubongo wa juu ambapo anaweza kufikiri sawasawa.
6. Adui wa kwanza wa wewe kuwashawishi wengine ni wewe mwenyewe. Ili uweze kuwashawishi wengine ni lazima wewe ushawishike kwanza. Ni lazima wewe ukubaliane na kile unachotaka wengine wafanye au wakupe. Ni lazima uweze kujidhibiti mwenyewe ili kuweza kuwashawishi wengine kuchukua hatua ambayo unajua ni muhimu kwao.
7. Ondoa chujio ambalo tayari unalo. Kila mmoja wetu ana chujio ambalo anatumia kuwachuja wengine kwa kadiri wanavyoonekana au walivyowazoea. Hivyo tunawapanga watu kwenye makundi kwa kufikiri tunawajua sana. Ili kuweza kuwa na ushawishi kwa wengine kwanza ondoa chujio hili na mwendee kila mtu bila ya kumhukumu, kuwa tayari kujifunza zaidi kutoka kwake. Usimweke mtu kwenye upande wowote, badala yake msikilize yeye kama yeye na hapa utaona njia bora za kuweza kumshawishi.
8. Kila kitu ambacho mtu anafanya, kuna sababu inayomsukuma kufanya. Hakuna mtu anayefanya kitu kwa ajali au kwa bahati mbaya pekee. Hivyo unapokutana na tatizo au changamoto kutoka kwa wengine, jua kuna kitu kimewasukuma kufanya walichofanya. Ili uweze kuwashawishi watu, jua ni kitu gani kinawasukuma wafanye kile ambacho wanafanya sasa na ni jinsi gani unaweza kuwafanya kuacha wanachofanya sasa na wafanye kile ambacho unawashawishi wafanye.
9. Mfanye mtu ajisikie ameeleweka. Ni lazima umwelewe mtu kabla hujataka kumshawishi afanye chochote unachotaka afanye. Jaribu kuvaa viatu vyake na mweleze wazi ya kwamba unaelewa kwa nini yupo pale alipo sasa. Na hata kama anafanya kitu ambacho anakosea, mwelewe kwamba kuna kitu kinasababisha yeye afanye hivyo. Usione kwamba yeye hayupo sahihi na kumweleza hivyo, ukienda kwa njia hiyo atakachofanya ni kujitetea na hutaweza kumshawishi kwa njia yoyote ile. Mwelewe mtu na atafunguka kwako.
10. Kama unataka wengine wajali kuhusu wewe, anza kujali kuhusu wao kwanza. Moja ya njia muhimu za kuweza kuwashawishi watu ni kuwafanya wavutiwe na wewe, wajali kuhusu wewe na hivyo wawe tayari kufanya kile ambacho unawaambia wafanye. Lakini hii haitakuja kwa wewe kukazana watu wavutiwe na wewe na wajali kuhusu wewe. Badala yake inakuja pale unapoanza kujali kuhusu wengine, na unapovutiwa na wengine.
Hivyo unapokutana na watu, usitumie nafasi hiyo kujisifia zaidi wewe, badala yake tumia nafasi hiyo kutaka kuwajua zaidi. Jua ni mambo gani wanafanya, changamoto gani wanapitia, yapi wameweza kukamilisha. Kadiri unavyojali kuhusu wao wanaanza kufunguka kwako na watakuwa tayari kufanya kile unachotaka wafanye.
[19/06/2016 01:25] Violeth: 11. Wafanye wengine wajione ni wa thamani. Hii ni mbinu muhimu sana unayotakiwa kuwa nayo kama unataka kuwashawishi watu kuchukua hatua fulani. Hakuna kitu ambacho mtu anapenda kama kuona amethaminiwa. Hii ndiyo maana watu wanapenda kuitwa mheshimiwa, bosi, mtaalamu, bingwa, na majina mengine yanayoonesha sifa za watu. Mfanye mtu aone ana mchango mkubwa kwenye kile anachofanya na kile unachotaka afanye ataweka mchango mkubwa pia. Kuwafanya watu wa thamani ni zawadi kubwa sana unayoweza kuwapa.
12. Epuka kueleweka tofauti na unavyotaka ueleweke. Katika harakati zako za kuwashawishi wengine, unaweza kuwa unatoa picha ya kinyume kabisa na kile ulichokuwa unataka kutoa wewe. Kwa mfano unataka watu wakuone wewe ni mwenye husara lakini kwao unaonekana ni mpumbavu. Au unataka wakuone ni mwaminifu ila wao wanakuona ni tapeli. Hali hii huwa inatokana na mtu kutokujiandaa vizuri na kutosikiliza wale ambao anataka kuwashawishi. Unahitaji kuwafuatilia kwa makini watu na kuona wanapokeaje kile ambacho unawapatia.
13. Kuna vitu vitatu ambavyo vinawasukuma watu kuchukua hatua, ukiweza kuvitumia vizuri vitu hivi utaweza kuwashawishi watu iwe ni kwenye kazi, biashara na hata kwenye familia.
Kitu cha kwanza ni mapenzi, hamu au shauku. Watu wapo tayari kufanya kile ambacho wanapenda kufanya na wana shauku kubwa ya kukifanya. Hivyo angalia ni kitu gani watu wanapenda na kitumie katika ushawishi wako.
Kitu cha pili ni hamasa. Watu wanapokuwa na hamasa wanakuwa tayari kuchukua hatua kwenye jambo lolote ambalo wanalipenda. Wafanye watu wahamasike kwenye kile ambacho unataka wafanye.
Kitu cha tatu ni fahari, watu wanaona ufahari pale wanapoona wamekuwa na mchango kwenye jambo fulani. Watu wanapoona kile walichofanya kina mchango kwa wengine wanafarijika sana.
Tumia vitu hivi vitatu kwa pamoja na utaweza kuwashawishi watu kuchukua hatua.
14. Uaminifu ni muhimu sana katika kuwashawishi wengine. Huwezi kuwashawishi watu kama hawakuamini na watu hawawezi kukuamini kama husemi ukweli na kutekeleza kile unachoahidi. Usiwe na haraka kwenye ushawishi wako, badala yake jenga mahusiano yenye uaminifu, kadiri watu wanavyokuamini, kutokana na matendo yako na siyo maneno tu, ndivyo wanavyokuwa tayari kukubaliana na wewe.
EPUKA WATU HAWA WA AINA TANO.
Japokuwa lengo la kitabu hiki ni kukupa mbinu za kuweza kuwashawishi watu, kuweza kuwafanya wakubaliane na wewe, kuna watu ambao hawashawishiki na wala hawawezi kukubaliana na wewe kwa lolote. Hawa ni watu ambao ni sumu kali na njia pekee kwako ni kuwaepuka haraka sana. Watu hawa wanajiangalia wao wenyewe sana na hivyo hawawezi kuwa tayari kufanya kitu ambacho kitawanufaisha wengine. Watu hawa wanaongozwa zaidi na ubongo wa chini na wa kati. Watu hao wa aina tano ni kama ifuatavyo;
15. AINA YA KWANZA; Watu ambao ni wahitaji na wategemezi kwako moja kwa moja (needy people). Hawa ni watu wazima, wenye nguvu zao na akili zao lakini wanakuchagua wewe ndiyo ubebe matatizo yao. Wanakuambia wazi kabisa bila ya wewe wao hawawezi kuishi na hivyo wanakutegemea kwa kila kitu. Hata maamuzi madogo ambayo wangeweza kufanya wenyewe hawafanyi mpaka wakusubiri wewe. 
Kama ingekuwa hivi tu wala isingekuwa shida, ila tatizo kubwa la watu hawa ni kwamba wanapenda kulalamika na watakulalamikia kwa kila kitu. Hata uwasaidie kiasi gani, ukikosea kidogo watakulalamikia kwamba umeharibu siku yao au maisha yao. Watataka wewe uache kila unachofanya ushughulikie matatizo yao na ukishindwa kufanya hivi watakulaumu kwamba huwajali.
Hawa ni watu ambao dakika moja watakuambia wewe ndiyo msaada mkubwa kao, na dakika inayofuata watakuambia wewe ndiyo umeharibu maisha yao.
Suluhisho; wakimbie haraka sana watu hawa, kaa nao mbali maana huwezi kuwasaidia kwa lolote. Haijalishi ni ndugu, rafiki au mtu gani, kama amekuwa na tabia hii na ukamweleza lakini habadiliki, kimbia haraka sana.
[19/06/2016 01:27] Violeth: 16. AINA YA PILI; Watu ambao ni waonevu (bullies). Katika maisha yako utakutana na watu ambao ni waonevu, na watakuonea sana. Hawa ni watu ambao wanataka wewe ufanye kile ambacho wanataka wao iwe unataka au hutaki. Hawajali kuhusu wewe wanachojali ni wao wenyewe. Na hawa watakuja wengi kuanzia ndugu, wenza, waajiri na hata washirika kwenye biashara.
Watu ambao ni waonevu wana tabia moja, huwa wanaenda kwa wale watu ambao wanaonekana ni wanyonge. Hivyo njia ya kuwaepuka hawa ni kukataa kuwa mnyonge. Usikubaliane kabisa na kile ambacho watu wanakulazimisha kufanya, hata kama ni mtu gani. Na waambie wazi kwamba hukubaliani na hilo na wakiona wewe ni mgumu watahamia kwa wengine. Kama ni mwajiri anakuwa mwonevu kwako, tafuta kazi nyingine.
17. AINA YA TATU; Watu ambao ni wapokeaji na wachukuaji tu(TAKERS). Hawa ni watu ambao wanajiangalia wao wenyewe tu, kila mara wanakuja kwako na shida ambayo wanataka uwasaidie na wanalalamika sana. Lakini siku wewe una shida ukiwaendea wana kila sababu ya kwa nini hawawezi kukusaidia. Watu hawa wanaona kama wao ndio wanastahili zaidi ya wengine. Watu hawa ni hatari sana kwako kwani wanaweza kuharibu mipango yako na ratiba zako kwa jinsi wanavyokuja na shida zao.
Njia ya kuondokana na watu hawa ni kuwa na kitu ambacho unataka wakufanyie. Pale anapokuja na kitu unataka umsaidie, mwambie sawa nitafanya hivyo ila na mimi nilikuwa naomba unisaidie hiki, (mwambie kitu ambacho unajua kabisa kipo ndani ya uwezo wake), atakimbia na hutamwona tena.
18. AINA YA NNE; Watu ambao wanajijali na kujisifia wao tu (NARCISSISTS). Hawa ni watu ambao wanafikiri duniani wao pekee ndiyo muhimu. Watu hawa huzungumzia zaidi mafanikio yao na kuona wengine kama hawajui wanachokifanya. Watu hawa ukiongea nao wanataka watawale mazungumzo kila unachowaambia wanakuonesha ni jinsi gani wao ni bora kuliko wewe. Watu hawa hawana shida na wewe ila pia hawajali chochote kuhusu wewe. Wanajiangalia wao tu. Waepuke watu hawa kwa kukaa nao mbali, kwa sababu hakuna namna unayoweza kuwashawishi, kwa sababu hawataki kusikia chochote kuhusu wewe, wanataka uwasikilize wao tu na kuwasifia.
19. AINA YA TANO; Watu ambao wana matatizo ya kisaikolojia, au ugonjwa wa akili (PSYCHOPATH). Hawa ni watu ambao hawana hisia zozote zile, wanachoangalia wao ni kile ambacho wanakitaka tu. Hawajui kama wanaumiza wengine na wala hawajali kama wanachotaka kitakuwa kibaya kwa wengine. Kwa tabia hizi watu hawa huwa na mafanikio makubwa kifedha na kikazi au kibiashara lakini kimaisha wanashindwa kwenda vizuri na wengine.  Unapokutana na watu wa aina hii kimbia haraka sana, usitake hata kujadiliana nao, maana wanapokuangalia hawaoni kingine bali ni jinsi gani watanufaika kupitia wewe hata kama wewe utaumia.
Waepuke watu hao wa ina tano na hakikisha wewe mwenyewe haupo katika moja ya aina hizo tano za watu. Kwa sababu badala ya kuwashawishi watu utakuwa unawafukuza kabisa.
20. Katika mipango yako ya kuwashawishi wengine kuwa makini sana usivuke mstari na kuwa mnyonyaji na mkandamizaji. Kuna tofauti ndogo sana kati ya ushawishi na ukandamizaji. Ushawishi ni pale ambapo unawawezesha watu kuchukua hatua au kufanya kitu ambacho kina manufaa kwao. Ukandamizaji ni pale ambapo unawawezesha watu kufanya kitu ambacho kina manufaa kwako ila kwao hakina manufaa au kinawaumiza kabisa. Kuna watu ambao wanaweza kutumia maneno yao vizuri na kuwakandamiza wengine, usiingie kwneye kundi hili.
Ni imani yangu kwamba umejifunza njia za kuongeza ushawishi wako kwa wengine na pia umejua yapi ya kuepuka.
Kama unavyojua, mambo haya yatakusaidia kama utayafanyia kazi.  Hivyo yafanyie kazi.
Kwa kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya Kiswahili tembelea MOBILE UNIVERSUTY, www.mobileuniversity.ac.tz Vitabu ni hazina, kila siku jifunze na fanyia kazi yale unayojifunza.

UNACHO TAKIWA KUFANYA UNAPOANZISHA BIASHARA

UNACHOTAKIWA KUFANYA PALE UNAPOANZISHA BIASHARA

Najua nazungumza na mabilionea wakubwa, kama si mabilionea wa sasa, basi ni mabilionea wa baadaye. Wewe ni bilionea, nakutamkia hili na unatakiwa kuamini pasipo kujali kwamba kwenye akaunti una shilingi elfu moja au chini ya hapo, unachotakiwa kuamini kwamba wewe ni bilionea.

Inawezekana umeanzisha biashara yako, kitu cha ajabu kabisa, fedha hazikai, kila ukipata leo, kesho hazipo, ili kuendesha biashara yako inakupasa kukopa sehemu, ni kweli ulipata faida, ila kwa nini ukope? Kopa wakati ukitafuta mtaji, ila kama umeshafanya biashara na faida ukapata, kwa nini ukope? Kwa nini usitumie faida uliyoipata kukuinua hapo ulipo?

Wengi wanakutana na hali hiyo, si wewe tu, hata mimi nilishawahi kukutana nayo, na si sisi tu, amini hata mabilionea wakubwa walishawahi kukutana na hali hiyo. Hivi unajua ni mabilionea wangapi waliwahi kufilisika? Unamjua Muitaliano Enzo Ferrari? Alipata fedha, akafilisika, akagundua alipofanya makosa, akatafuta tena, akazipata.

Wewe kama binadamu wengine, unaweza kupata fedha na kufilisika, hapa siwazungumzii wakina Bakhresa, Mengi na wengineo, nakuzungumzia wewe mwenye biashara ndogo, nataka biashara yako ikue, utoke hapo ulipo na usogee mbele zaidi, ufanikiwe na siku moja uitwe bilionea Omari, Selemani, John, Hamisi, Sara, Anna, Peter au jina lolote ulilokuwa nalo.

Hizi ni baadhi ya njia ambazo zinaweza kukusaidia kufikia ubilionea japokuwa una biashara ndogo au kipato kidogo.

1. WEKA MALENGO: Kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya kama mfanyabiashara ni kuweka malengo. Hebu chukua karatasi, andika malengo yako na kuyafanyia kazi. Kumbuka wewe ni bilionea, usiweke malengo ambayo unadhani kwamba pia ua utayafikia, ukiyaandika hayo, jua hautotoa nguvu kubwa kupambana ili uyafikie malengo hayo. Kama una mtaji mdogo, weka malengo makubwa ya kufanikiwa, unapoweka malengo makubwa zaidi ya ulichonacho kitakufanya ujitoe zaidi, uongeze juhudi ili kufikia kile unachokiwazia.

Mfano wewe ni mfanyabiashara mdogo, ukaweka lengo kwamba mpaka mwaka kesho lazima uanzishe biashara ya kuuza mahindi mitaani. Sawa, si vibaya lakini ulitakiwa kuweka malengo ya biashara kubwa zaidi. Kwa fedha hizohizo ulizokuwa nazo, unaweza kuanzisha biashara ya mahindi, ukijiwekea hivyo, jua kwamba unayachelewesha mafanikio yako. Ninataka ujitume kwa nguvu zote, ukiweka yale malengo makubwa, utajiona huwezi kufika lakini ndiyo yatakayokufanya kupambana zaidi, hutolala, utapambana usiku na mchana ila ukiweka lengo dogo, utasema subiri upumzike kwani lengo hilo litakuja hata kama hutojitoa, hivyo ili ufanikiwe, jiwekee lengo kubwa na hakika utapiga hatua.

Mfano mzuri mimi. Sikuwa na fedha kipindi cha nyuma, ishu ya kuanzisha magazeti ilihitaji msingi mkubwa sana, ila sikutaka kukwepa lengo langu la kufanya hivyo. Ningeweza kusema niuze machungwa mitaani, kweli ningeuza, lakini kwa nini niweke lengo dogo? Je ningejitoa zaidi? Ili nijitoe, ili nifanye kazi usiku na mchana ilikuwa ni lazima niweke lengo kubwa, nikaweka, nikajitoa na kufanikiwa. Kama Shigongo, yule mtoto masikini ameweza, vipi kuhusu wewe?

2. USIOGOPE KUFELI: Ndiyo! Kuna watu waoga sana, wanaogopa kufanya biashara fulani kubwa kwa kuwa wanaogopa kuanguka. Rafiki yangu, kuanguka ni sehemu moja ya maisha, ili usonge mbele ni lazima uanguke. Huwezi kujua kuendesha baiskeli kama hujaanguka, ni lazima uanguke ili ujue, iko hivyo.

Mtoto anapoanza kutembea, kuna kipindi anaanguka, mbona yeye hakati tamaa na kusema kwamba kuanzia leo hatembei tena kisa ameanguka? Akianguka, hunyanyuka na kutembea tena, akianguka anajaribu tena.

Wewe kama mfanyabiashara mdogo au mkubwa, jifanye mtoto, usiogope kufeli, ili usonge mbele, ni lazima ufeli, huwezi kuwa mshindi siku zote, kuna kipindi unashindwa, ukishindwa, unakaa chini na kuwaza umeshindwa wapi, unajipanga na kurudi tena kwenye gemu.

Kama ningekuwa naogopa kufeli, nakwambia ukweli kwamba nisingekuwa hapa, labda leo ningekuwa mtaani tu nafanya biashara ndogondogo, kuogopa kufeli kungenifanya niwe kulekule nilipokuwa nyuma. Ili ujifunze, ili upige hatua ni lazima ufeli, ukifeli, unajifunza na kusonga mbele.

3. WEKA UMAKINI NA FEDHA ZAKO: Siku zote nimekuwa nikiwaambia watu, si vizuri kutumia kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya unachoingiza. Mwingine ana biashara inaingiza elfu ishirini kwa siku, ila anataka kufanya matumizi yasiyokuwa na faida kwa kutumia elfu thelathini. Ndugu yangu! Huwezi kuishi kwa maisha haya halafu ukaja kufanikiwa. Unatakiwa kuwa makini na fedha zako.

Mwingine anasema, nimepata faida nyingi, acha nikale bata! Ndugu zangu, bata haziishi, kila siku zinaongezeka, baa hazifungwi, umezikuta na utaziacha, kumbi za starehe kila siku zinafunguliwa mpya.

Ithamini pesa yako, hata kama ni shilingi hamsini, ithamini. Unapokuwa na elfu moja, inayokamilisha hela hiyo ni shilingi hamsini, kama ukiwa na 950, huwezi kupata 1000 kama huna hamsini, kwa hiyo kwenye maisha yako ya kibiashara, hata shilingi 50 ni muhimu mno kwako.

Usiipuuzie fedha yoyote ile, panga matumizi yako ya kawaida, si muhimu sana kunywa soda kama huna sababu ya kufanya hivyo! Hakuna umuhimu wa kula chipsi kuku kama hakuna umuhimu wa kufanya hivyo! Kwani usipokula chipsi kuku utakufa? Kama una kiasi kidogo cha fedha basi hata matumizi ya fedha yako hakikisha yanakuwa madogo na si makubwa zaidi ya kile ulichokipata.

4. JENGA URAFIKI NA WENYE FEDHA: Hapa simaanishi kwamba wasiokuwa na fedha inabidi watengwe, hapana! Ila unatakiwa kuwa makini, ni vizuri kutengeneza marafiki wapya lakini inabidi uwe makini. Kabla ya kuwa nilivyo niliwahi kuwasikia watu wakisema unapoanza kufanikiwa unabadilika, nilipinga lakini nikaja kuona inawezekana.

Unapokuwa umefika hatua fulani, automatic unaanza kutafuta watu ambao wanaweza kukuvusha kutoka hapo ulipo, watu wenye uwezo wa kukufanya kufanikiwa zaidi. Kumbuka shuleni kwenu, ni wanafunzi wangapi waliokuwa na akili walikuwa marafiki wao kwa wao? Kwani hawakuwa marafiki zako pia, walikuwa marafiki zako ila wenyewe wakawa beneti, ipo hivyo.

Unapopata fedha, unapofanikiwa, jaribu kutengeneza ukaribu na watu waliofanikiwa, usiwaache wale wengine, kuwa nao ila usiwe nao beneti kupindukia, kama unaona mtu haeleweki, hana hamasa ya kukufanya kufanikiwa, kwa nini uwe naye beneti? Muache awe rafiki wa kupiga naye stori dakika kumi na kuondoka.

Unapokuwa siriazi kutafuta fedha, huna budi kuwatafuta waliofanikiwa, wakufundishe kwa nini wapo hapo, walipitia nyanja zipi mpaka kufanikiwa hivyo? Ni lazima ujifunze kupitia wao na hakika utafanikiwa.

5. USICHANGANYE BIASHARA NA URAFIKI/NDUGU: Ndiyo! Wengi tunafeli hapa. Tunapopata nafasi ya kufanya biashara, wengi tunakosa kufanikiwa kwa sababu tu tumechanganya urafiki katika biashara. Biashara ndogo lakini bado unataka kukopesha, tena kwa watu ambao huna uhakika kama watakulipa.

Unapoanzisha biashara, wengi watakuja kukopa na si kununua, hebu jiulize, wakati hujaanzisha hiyo biashara, mbona hawakuwa wakienda kukopa sehemu nyingine? Jua sisi binadamu tuna makusudi, tunapomuona mtu ameanzisha biashara, mara nyingi tunataka kumuangusha chini ili tumcheke, tumdhihaki kwamba kiko wapi sasa! Unatakiwa kuwa makini sana, huu si muda wa kupeleka urafiki na undugu katika biashara. Unapoanzisha biashara na ikatokea umemuajiri ndugu yako, mwambie wazi kwamba upo kama mfanyabiashara na si kama ndugu, anapofanya makosa, mchukulie hatua kama unavyomchukulia mtu baki, ukimuacha kwa kuogopa lawama, huyohuyo baadaye atakuja kukucheka.

Unapoona una hamu ya kula chipsi, na wewe unaifanya biashara hiyo ya chipsi, nunua chipsi zako, si kwamba ni zako basi na wewe ule bure. Najua ni ngumu kwa watu wengine lakini inabidi ufanye hivyo ili kuifanya biashara yako isimame.
Leo unapouza chipsi na kula bure, amini kwamba kesho utataka uongeze na chipsi yai, keshokutwa chipsi samaki, sasa ukifanya hivyo, hutofanikiwa kwa hiyo ni lazima hata wewe mwenyewe ujidai.

Sina mengi, ila tukutane muda mwingine kwa makala nyingine ya ujasiriamali. Kumbuka, wewe ni bilionea, fanya mambo kama bilionea.

SHARE, LIKE kadiri uwezavyo ili na marafiki zako wajifunze.

MUNGU AKUBARIKI.

FAIDA ZA BIASHARA YA MTANDAO

WATU WOTE WA NAPENDA KUISHI MAISHA MAZURI HIVYO FUATILIA KWA KINA

FAIDA 10 ZA KUFANYA BIASHARA YA MTANDAO

Biashara ya mtandao ni moja ya biashara zinazokua kwa kasi kubwa zaidi katika karne tuliyo nayo sasa. Imeonekana kuwa makampuni yanayofanya biashara hizi yana tabia ya kukua kwa kasi sana na kudumisha ukuaji huo kwa muda mrefu zaidi kuliko makampuni ya biashara za kawaida.
Hadi kufikia 2011, biashara za mtandao zilikaridiwa kufikia kuwa na thamani dola bilioni 100 zikiwa zinatengeneza faida kubwa sana. Haikushangaza kumsikia tajiri mkubwa duniani, Bill Gates, anayemiki kampuni ya software za kompyuta akisema kuwa kama ataruhusiwa kuanza upya biashara, atafanya biashara ya mtandao (network marketing). Katika mada hii tutazizungumzia faida za kufanya biashara hizi za mtandao.
Lakini kabla ya kuanza kuziorodhesha faida hizo tupate maneno machache kuhusu tabia ya biashara hii. Watu wengi huchukulia kwamba biashara hizi ni kimbilio baada ya kushindwa vitu vingine. Napenda kuwashauri kuwa hizi ni biashara kama nyingine zo zote, zinahitaji uwekezaji wa muda, nguvu na pengine pesa. Zina tabia tofauti kidogo na biashara zingine au kazi nyingine za ajira. Wakati hazihitaji mtu kuwa na cheti cha masomo, zinahitaji mwanachama
kuwa na tabia tofauti kidogo na ya mtu aliyezoea kuajiriwa. Hizi ni biashara ambazo mtu anayeshiriki atakuwa mwamuzi wa kila jambo linalohusu biashara yake, akishaanza kufanya biashara hii hakutakuwepo na mtu wa kumsukuma.
Kwa hiyo, zinahitaji mtu awe na uwezo wa kuwa na maamuzi sahihi na kufanya kazi kwa kujipangia mwenyewe. Watu waliofanikwa mapema na kwa kiwango cha juu ni wale waliokuwa na morali ya juu, waliofanya kazi bila kupumzika wakiwa wamejiwekea malengo yao. Hizi ni biashara ambazo unatakiwa kila wakati uzifikirie na kufanya jambo fulani kusogeza gurudumu lako mbele. Unatakiwa kujifunza sana kutoka kwa wale waliokutangulia na wengine wengi
waliokwisha fanikiwa katika biashara hizi.
Kwa vile ni biashara ambazo hazileti utajiri ghafla, zinahitaji uvumilivu wa hali ya juu mwanzoni na kusimama kwenye malengo uliyojiwekea bila kuyumba. Zina tabia ya kuanza kuonyesha matunda taratibu na kuongeza kasi kadiri unavyopanda ngazi kwenye kampuni yako. Ukifika juu, uzito wa kazi hupungua na unaanza kuishi kwa mtindo wa maisha waishio matajiri na watu walio maarufu.
Sasa tuone ni faida gani zinapatikana kutokana na kufanya biashara hizi za mtandao. Kuna faida nyingi sana za kufanya biashara ya mtandao, lakini katika ukurasa huu tumechagua na kuelezea faida 10 tu:
Hii ndio faida kubwa kuliko zote na ndiyo maana hapa nimeiweka kuwa ya kwanza. Hebu fuatilia kwa nini nasema hivyo…..
Katika siku moja idadi ya saa inaeleweka na huwezi kuibadili. Katika saa hizo za siku moja unatakiwa ufanye kazi ya kukupatia kipato, upate muda wa kulala, upate muda wa kuwa na familia na muda mwingine kwa ajili ya shughuli zako nyingine.
Watu wengi wanatakiwa kuwepo mahali walipoajiriwa kwa saa 8 kwa siku … kwenye kazi ambayo wanaifanya tu hata kama hawaipendi. Kwa kubadilishana na muda wao, waajiri huwalipa kiasi fulani cha pesa kwa kila saa aliyokuwepo kazini au kulingana na idadi fulani ya vitu alivyovizalisha. Hakuna malipo ya zaidi ya hapo. Kipato cha mwajiriwa huyu kimefungwa au kimewekewa ukomo kwa sababu;
Kwanza: Kuna ukomo wa idadi ya saa za kufanya kazi, na
Pili: Kuna ukomo wa idadi ya vitu unavyoweza kuvizalisha wewe peke yako katika muda uliopangiwa.
Kwa upande wa pili, tutazame biashara ya mtandao.
Biashara za mtandao huwalipa wanachama wao kutokana na kazi za wanachama wengine. Kwa hiyo basi, mwanachama ambaye ameweza kuongeza idadi ya wanachama walio chini yake atalipwa zaidi, na kila atakapowaongeza zaidi, atazidi kulipwa zaidi.
Uzuri uliopo hapa ni kuwa unaweza kuongeza idadi ya wanachama chini yako bila kuhitaji kuongeza muda wako wa kufanya kazi. Unaweza kupunguza muda wa kufanya kazi na bado ukaona kipato chako kikiongezeka. Ulipwaji kutokana na watu uliowasajili chini yako na kuwafundisha (leveraged income) ndio unaoifanya kuwa faida ya kwanza kwenye orodha hii.
Kampuni za mtandao zinawapa fursa wanachama wao kupata malipo endelevu kwa kazi walizozifanya mara moja. Karibu kila mmoja wa watu wanaojiunga na biashara hizi huwa amevutiwa na aina hii ya malipo. Wewe kama mwanachama unamsajili mwanachama mara mmoja tu na mtu huyu akiendelea kununua bidhaa na kujenga timu inayofanya kazi vizuri, wewe utaendelea kulipwa tena na tena bila ushiriki wako wa moja kwa moja.
Unaweza kuanza biashara ya mtandao kwa mtaji mdogo sana au kwenye kampuni nyingine bila kuwa na mtaji kabisa. Hakuna tofauti kati ya yule aliyenza na mtaji mdogo na yule aliyeanza na mtaji mkubwa, fursa zenu za kufika mnakotaka zinafanana na kubwa kuliko fursa utakayopata kwenye mifumo mingine ya biashara.
Pamoja na kuwa pengine utaanza biashara yako bila mtaji wo wote, utahitaji kiasi fulanai cha pesa kwa ajili ya uendeshaji wa biashara yako ikiwa ni pamoja na kununua bidhaa, mawasiliano, usafiri, matangazo n.k.
Nchini Tanzania, kuna baba ambaye alianza biashara kwa kutoa kiingilio kidogo kwenye kampuni ya FOREVER LIVING PRODUCTS  (kampuni inayohusu bidhaa za afya ya binadamu)     akiwa hana elimu yeyote hata kusoma ilikuwa shida akiwa anafanya biashara ya kuuza  genge Maeneo ya TANDIKA  Dar es salama TANZANIA pia alikuwa na mgogoro na mmiliki wa nyumba aliyopanga kwani  alikuwa anachelewesha kodi ya nyumba. akaanza kwa kupeleka wagonjwa (wateja wake wa Mbogamboga waliochukua ili kuhifadhi afya zao) kupata maelekezo ya virutubisho kutoka kwenye kampuni hiyo Kisha nao wakavutiwa wanaojiunga chini yake, na kukua taratibu hadi kufikia kupata bonasi nzuri kila mwezi na  akaweza kujengakatika nyumba nzuri kipindi kifupi tu – hakuwa na mtaji zaidi ya pesa ya kiingilio.
Kampuni nyingi za mtandao zinaruhusu wanachama wao kufanya biashara kimataifa. Hili linawezekana kwa kutumia mtandao. Unaweza kumsajili mwanachama kutoka nchi yo yote duniani na ukapata kipato kitakachotokana na kazi anayoifanya mwanachama huyu huko aliko. Kwa hiyo unaweza kujijengea biashara kubwa,
katika nchi tafauti, wewe ukiwa ndani ya nyumba yako.
Biashara za mtandao hazihitaji uwe na uzoefu wa kuuza, wala hazihitaji uwe umepata mafunzo ya biashara. Kuwa na uzoefu huo au mafunzo hayo ni kitu kitakachokusaidia, lakini kila mwanachama anayejiunga na biashara hizi hupewa mafunzo ya kutosha. Mafunzo hayo utayapata kutoka kwenye kampuni au kutoka kwa mtu wa juu
yako (aliyekusajili). Kampuni nyingine hutoa mafunzo ya aina mbali mbali kwa wanachama wao, hutoa mafunzo darasani, CD, DVD, vipeperushi na hata vijitabu vya kujisomea.
Kitu kibaya sana kwenye biashara za aina nyingine ni kukosa uhuru na hasa uhuru wa muda. Kazi nyingi zinakutaka ufanye kazi – saa 9 kwa siku, siku 5 kwa wiki – na unapata kipato kwa kuuuza muda huo kwa wiki. Huwezi kujiamulia ufike kazini saa ngapi. Mwajiri wako ndiye anayekupangia nini cha kufanya na wakati gani ukifanye.
Biashara ya mtandao unakuondolea vikwazo vyote hivi. Kuanzia siku ya kwanza unapoanza biashara ya mtandao, unajipangia ufanye kazi na nani… utakataka ufanye kazi muda gani… na utapenda kufanyia wapi kazi yako.
Una uchaguzi wa namna utakavyopenda kufanya biashara yako: kuongea na watu moja kwa moja; kutumia barua pepe; kutumia simu yako ya mkononi, kuitisha mikutano n.k. Ni biashara yako na utaifanya unavyopendezewa ifanyike.
Moja ya faida kubwa ya biashara za mtandao ni kujiendeleza kibinafsi. Wafanya biashara za mtandao ni viongozi makini. Katika kufanya biashara hizi utajiongea ujuzi mwingi na uzoefu mkubwa katika kuzungumza mbele ya kadamnasi, kutoa ushauri, kufundisha watu na namna ya kuishi na watu.
Kufanya biashara ya mtandao kunakuwezesha kufahamiana na watu wa mikondo mbalimbali ya kimaisha, kujipatia marafiki wapya na kujua mikondo mingine ya kibiashara.
Hakuna kiwango cha mapato unachopangiwa kupata. Katika kazi au biashara nyingine za kawaida kiwango chako cha mshahara kimepangwa na hakiwezi kuwa zaidi kwa elimu na ujuzi ulio nao.
Hivyo sivyo katika biashara za mtandao. Wewe ndiye utakayejipangia kiwango unachopenda kukipata, kampuni haina
pingamizi la namna yo yote kama ilivyo kwenye makampuni ya kawaida.
Ukishapata ujuzi wa kufanya biashara ya mtandao, utapata kipato cho chote kulingana na uvumilivu wako na kujituma kwako katika kuwasaidia wengine.
Maendeleo ya teknolojia yanamwezesha mfanya biashara ya mtandao kufanya shughuli zake po pote alipo. Ukiwa na simu ya kiganjani unaweza kuwasiliana na wateja wako kutoka po pote ulipo.
Ukiwa umeunganishwa kwenye internet, unaweza kuchukua simu yako au lap top yako na ukaendelea kufanya biashara zako ukiwa safarini, ukiwa kwenye mapumziko, ukiwa umekwenda kuwaona ndugu walio kwenye mji mwingine na hata ukiwa nchi nyingine.
Baadhi ya bidhaa na huduma bora kabisa ulimwenguni hupatikana kwenye makapuni yanayofanya biashara ya mtandao. Bidhaa hizi haziuzwi kwenye maduka ya kawaida, na hata kama zingeuzwa
humo, hakuna mtu ambaye angezitambua. Bidhaa ikiwa ni nzuri na ya kipekee, inahitaji mtu wa kuielezea, jambo ambalo haliwezekani dukani kutokana na uwingi wa bidhaa katika duka hilo.
Ni yule mtu aliyetumia bidhaa au huduma akaipenda, anayeweza kuuelezea uzuri wa bidhaa au huduma hiyo.
Katika mada yetu ya leo tumeona faida 10 zinazopatikana kwa kufanya biashara za mtandao.

SAFARI YA MAFANIKIO

JE,IPI SAFARI YAKO YA MAFANIKIO UMEPANGA KUPITIA MAANA ZIPO NYINGI

IJUE Orodha Mpya Ya Mabilionea; Mambo Kumi Ya Kuzingati Ili Na Wewe Uweze Kuingia Kwenye Orodha Hii Siku Za Baadae.
Jarida maarufu kwa kufuatilia watu matajiri duniani hivi karibuni limetoa orodha mpya ya watu matajiri sana duniani. Katika orodha hii mpya, mmiliki wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates amerudi kwenye nafasi ya kwanza na kuwa mtu tajiri kuliko watu wote duniani. Gates ana utajiri wa dola za kimarekani bilioni 79.2
Orodha hii ya 29, inaonesha kwamba duniani kuna jumla ya mabilionea 1826 na kwa mwaka jana tu mabilionea wapya 290 wameingia kwenye orodha hii. Pia vijana hawajaachwa nyuma, kwani mabilikonea 46 wana umri chini ya miaka 40.
Katika orodha hii ya mabilionea, 29 wanatoka Africa na hata hapa Tanzania tunaye bilionea ambaye ni Mohamed Dewji.
Orodha hii ya mabilionea inamengi sana ya kujifunza ambayo yanatuonesha kwamba nafasi hizi sio kwa ajili ya watu wachache tu. Bali kwa yeyote anayetaka kufikia nafasi hizi anaweza na hata anayezifikia hahakikishiwi kuwepo hapo milele.
Leo katika makala hii tutajadili mambo kumi muhimu ya kuzingatia ili na wewe uweze kuingia kwenye orodha hii miaka ijayo. Mimi tayari nina mpango huo na najua hakuna kinachoweza kunizuia, kama na wewe una mpango huu karibu uongeze mbinu zitakazokusaidia. Kama huna mpango huu pia endelea kusoma na unaweza kuuweka au hata usipouweka bado utakuwa umejifunza mambo muhimu yatakayotatua matatizo yako ya kifedha.
SOMA; Kama Unafikiri Huwezi Kuwa Bilionea Soma Hapa Na Uanze Kuelekea Kwenye Ubilionea.
1. Amini kwamba inawezekana wewe kuwa bilionea.
Hatua ya kwanza kabisa ya wewe kuweza kuwa bilionea ni kuamini kwamba inawezekana. Maana kila kitu kwenye maisha kinaanza na imani. Kama unaamini unaweza ni kweli utaweza. Kama unaamini huwezi ni kweli hutaweza na hakuna atakayeweza kukulazimisha.
Kubali sasa kwamba unaweza kuwa bilionea na amua kuwa bilionea hayo mengine utajifunza ndani ya safari.
2. Mshahara hauwezi kukufikisha kwenye ubilionea.
Kama umeajiriwa unaweza kuchukuia hili ila ndio ukweli wenyewe. Mshahara hauwezi kukufikiasha kwenye ubilionea, sahau kabisa ndugu yangu. Niliangalia kwenye orodha hii ya forbes katika mabilionea 1826, 119uh ni wajasiriamali, yaani wametengeneza ubilionea wao wenyewe. 230 wamerithi utajiri wao na 405 wamerithi sehemu ya utajiri wao na wanaufanyia kazi kuukuza zaidi. Moja kwa moja wewe huwezi kurithi ubilionea kwa hiyo umebakiwa na njia moja tu, UJASIRIAMALI.
SOMA; Njia Nne Za Uhakika Za Kufikia Utajiri, Angalizo; Ajira Sio Mojawapo.
3. Chagua kitu kimoja, au vichache vya kufanya.
Ukiangalia orodha hii ya forbes, asilimia kubwa ya mabilionea wanafanya vitu vichache sana. Kwa mfano Bill Gates anamiliki kampuni ya kutengeneza program za kompyuta, Warren Buffet ni mwekezaji, Aliko Dangote yupo kwenye viwanda.
Ni muhimu sana wewe kuchagua kitu kimoja au vichache unavyopenda kufanya na uvifanyie kazi kwa juhudi na maarifa ili uweze kufikia mafanikio makubwa na utajiri.
4. Usichukie mabilionea.
Baada ya orodha hii kutoka, vyombo mbalimbali vya habari viliweka kwenye mitandao yao ya kijamii na wananchi wakaanza kutoa maoni yao. Wengi walikuwa wanatoa maoni ambayo ni ya hasira dhidi ya mabilionea hawa. Wengi walisema kwamba ni watu ambao ni wabinafsi, hawajali, wana fedha nyingi wakati watu wengine wanakufa njaa na kadhalika. Huenda na wewe una mawazo kama haya, sasa nakwambia mawazo hayo yanakurudisha nyuma. Kwa kuwachukia mabilionea unajizuia na wewe mwenyewe usiwe bilionea. Mambo mengi yanayosemwakuhusu mabilionea ni ya uongo. Soma namba tano hapo chini.
5. Wasaidie wengine.
Kutoa misaada ni moja ya mambo yatakayokuwezesha kufikia ubilionea. Watu wengi na huenda wewe ni mmoja wao wameaminishwa kwamba mabilionea ni watu ambao wanajali fedha zao tu na hawajali masikini. Lakini tukianza na mtu tajiri kuliko wote duniani, Bill Gates ndio mtoa msaada mkubwa duniani kupitia taasisi yake ya BILL AND MELLINDA GATES FAUNDATION. Taasisi hii imesaidia watu wengi sana huku africa na hata hapa Tanzania inafanya kazi. Unahitaji kutoa sehemu ya utajiri wako kwa watu ambao hawajiwezi na utapata utajiri mwingi zaidi.
Siri ya kupokea ni kutoa.
SOMA; Tumia Siri Hii Moja Kupata Chochote Unachotaka Kwenye Maisha Yako.
6. Fanya kazi kwa juhudi na maarifa.
Tabia ya kutega tega kazi haiwezi kukufikisha kwenye ubilionea. Na kwakuwa tumeshakubaliana kwamba ajira haiwezi kukufikisha kwenye ubilionea, unahitaji uwe mtu wa kujituma sana ili uweze kufanikiwa kwenye ujasiriamali. Unahitaji kujua vizuri kile unachofanya na kukifanya kwa ubora wa hali ya juu sanakuliko watu wengine wote walivyowahi kukifanya hapa duniani.
7. Usiridhike na mafanikio kidogo.
Hii ni sumu kubwa kwa watanzania kufikia ubilionea. Mtu anakuwa na biashara inayompatia faida kubwa kuliko wengine wanaomzunguka anaanza kujiona yeye yuko mbali sana. Anaanza kula starehe, kununua magari ya kifahari ambayo hayahitaji, kununua majumba makubwa ambayo hayamzalishii na vitu vingine vingi vya kujionesha. Sikiliza, hakuna wakati ambao unaweza kusema kwamba mimi ndio nimeshayaweza maisha, mimi nimeshakuwa mshindi, wakati huo utakaokubali hivyo ndio wakati ambao utaanz akuanguka, ndio wakati ambao utaanza kushindwa.
Usiridhike na mafanikio kidogo unayopata, endelea kuboresha zaidi na zaidi.
8. Soma, soma, soma.
Nafikiri hiki ni moja ya vitu ambavyo ni muhimu sana kuliko hata hivyo tulivyojadili hapo juu. Maana hata kama huna sifa tulizojadili hapo juu na hata kama hutaki kuwa nazo kwa kuanza kusoma leo, na kuendelea kusoma kila siku utashangaa unaanza kujijengea sifa hizo.
Siku moja mwanafunzi anayemaliza chuo alimuuliza Warren Buffet ni kitu gani anaweza kufanya ili na yeye awe tajiri sana. Warren Buffet alichukua karatasi na kumuonesha akamwambia, soma karatasi 500 kama hizi kila siku. Warren ni mzee, ana miaka 84 ila asilimia 80 ya muda wake wa kazi anautumia kusoma. Hii inamfanya aone ni kampuni gani zinafanya vizuri na kuweza kuzinunua, kusoma kumempa faid akubwa sana kuliko wengine ambao hawasomi kama yeye.
SOMA; Kama Hutajifunza Chochote Mwaka Huu Basi Jifunze Hiki Kimoja Tu
9. Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA.
Hili ni eneo muhimu ambapo utapata nafasi ya kujengewa misingi yote muhimu itakayokuwezesha wewe kuwa bilionea. Utajifunza kuhusu biashara na ujasiriamali, utajifunza kuhusu tabia za mafanikio , utapata uchambuzi wa vitabu mbalimbali ambavyo vitakubadili mtazamo wako na kukuongezea maarifa na kikubwa zaidi utapata nafasi ya kuwa kwenye kundi la wasap ambapo unakutana na watu wengine wanaoelekea kwenye ubilionea kama wewe. Yote hayo ni kwa ada ya tsh elfu 50 tu kwa mwaka. Kujiunga bonyeza maandishi haya KISIMA CHA MAARIFA.
SOMA; Faida Kumi Za Kujisomea Ukiacha Kuongeza Maarifa.
10. Soma sana vitabu mbalimbali  na tafuta connection  na watu  waliofanikiwa pia  ili Kupata mwongozo sahahi.