Morning Rise Up
✍"Fimbo iliyo mkononi Ndiyo iuayo nyoka ".
Wakati nasoma methali hii sikuwa naielewa hasa nikijiuliza kuwa kama nyoka atakuwa mkubwa Mfano wa chatu na mimi nikiwa na fimbo Ndogo Je nitaweza kumuua nyoka??.
Ilikuwa ngumu sana kuielewa methali hii na nilimsumbua sana mwalimu wangu ili nielewe vizuri. Asante sana kwa Mwalimu kunivumilia kwa maswali ambayo yalilenga mimi kuelewa zaidi.
Mwalimu alinieleza kuwa "Joas Hata kama utakutana na chatu,silaha ya kwanza utakayo tumia ni ile itakayo kuwa mkononi mwako huku ukitafuta silaha kubwa." aliendelea kusema "Hata kiatu ulichovaa chaweza kumuua nyoka ".
Ukweli ni kwamba tumewaza kufanya makubwa ,lakini tumeshindwa kwa sababu Hatuwezi kuvitumia vile vidogo tulivyonavyo kwanza kwa muda huo huku tukisubiri vikubwa.
Kuna mtu ana kipaji ambacho hata hakihitaji mtaji, lakini mtu huyu kakaa tu akisubiri fedha za muujiza maisha yaanze Kubadilika. Je, Unachukua hatua gani kuonesha jamii kama una kipaji ili jamii ikukubali au umekaa tu ukisubiri mtu aje akutoe Mahali ulipo⁉ Nasikitika kwamba haitawezekana mpaka hapo Wewe utakapochukua hatua stahiki ya kufanya chochote Unachoweza kufanya
Hivi unajua Masanja Mkandamizaji alikotoka?Je,asingetumia kipaji chake nani angemuona?? .Hivi Unamjua Mbwana Sammatta⁉ Leo Mbwana Sammatta analipwa mshahara kwa mwezi zaidi ya pension(mafao) yako utakayolipwa baada ya kustaafu kwa kuwa alitumia kipaji alichokuwa nacho.
Unaweza Nini⁉ Unapenda kufanya nini⁉Hujui kuna watu ni matajiri kwa uchoraji⁉ Hujui kuna watu ni matajiri kwa kukimbia (riadha),hujui kuimba ni utajiri⁉ .Shida umedharau uwezo wako ambao unaweza kukutajirisha.
Unasubiri nini⁉ Unasubiri mtaji mkubwa⁉ Unasubiri msaada toka nje⁉ .Anza na kinachowezekana huku ukisubiri hayo makubwa unayofikiri.
Hakuna nyumba ambayo haikuanza na msingi ikiwepo itakuwa ya mchawi.Hivi Kuna Chuo kikuu Bila shule Ya msingi⁉ .hivi Kuna magunia ya Karanga ambayo hayakutokana na uaminifu wa mkulima kupanda Kile alichokuwa nacho⁉.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni