Ijumaa, 29 Julai 2016

NJIA ZA MAFANIKIO

TAMBUA NJIA ZA MAFANIKIO.

Natumaini hujambo,msomaji wa makala hii.Leo tutazungumza njia za mafanikio ktk maisha yetu ya kutafuta.

Mafanikio yapo mengi,kuna mafanikio ya kibiashara,kielimu,kijamii na kisiasa yote yanaongozwa na mbinu zifuatazo kwa kutawaliwa na utayari wako.

~KUJITAMBUA,jitambue wewe ni nani,unafanya nini,jamii inanufaika kwa uwepo wako? walio wengi bado hawajajitambua kutokana na mfumo wa maisha ya jamii unayoishi wengi wanafikiri kujitambua baada ya umri kua umetupa mkono.Ni lazima utambue uwezo wako ktk kupambanua mambo ya mafanikio na utambue jinsi gani utaweza kuisaidia jamii kutokana na kujitambua kwako,Hivyo anza leo kujitambua wewe ni nani,kwanini unaishi hivyo? Unaonaje jamii ikinufaika kwa kujitambua kwako?

~JITOFAUTISHE,mara baada ya kujitambua sasa anza kujitofautisha kutoka makundi ya watu wasio jitambua kwasababu unapoendelea kuchangamana nao utakua hujabadili kitu,utakapokua umejitofautisha sasa wenzio wataiga mfano wako hata wasipo kuambia lakini utaona tu,kumbe kwa kujitambua kwako na kujitofautisha kwako tayari utaokoa maisha ya wengi ambao walikua wameanza kupotea.Tayari utaanza kuisaidia jamii kutokana na kujitofautisha kwako.

~TAFUTA KITU CHA KUKUUNGANISHA NA JAMII YAKO,unaweza kutafuta shughuli itakayo kuunganisha na jamii yako.Kwa mfano tafuta biashara itakayogusa maisha ya jamii kutokana na huduma utakazo toa,tafuta kazi ambayo itakukutanisha kila siku na jamii yako,unaweza kukutana na jamii kwa njia nyingi ambapo kwa njia hizo itakusaidia wewe kubadili maisha ya wengi kuanzia mitazamo hadi uhalisia wa maisha yao ya kila siku.

~KUMBUKA KUJALI MUDA,mara nyingi muda ndio kila kitu kwako katika kukamilisha safari ya mafanikio utaamua mwenyewe kwa muda gani ufikie kilele cha mafanikio,inapendeza sana kuwa mtu wa kujali muda hasa kutumia muda kwenye shughuli za mafanikio.Umri sio rafiki kumbuka leo ni yako na sio kesho tunza muda uvune matunda yake.Sio lazima ushinde kazini au kwenye biashara lakini tambua hata sekunde moja kwako ni mali kwasababu unaweza kuamua kufanya kitu kizuri cha kubadili maisha yako iwe kwa mtazamo au uhalisia.

~TAMBUA MCHANGO WA MARAFIKI,marafiki wanaweza kubadili maisha yako kua mazuri sana,mazuri kiasi,mabaya na mabaya sana.Hivyo chunguza kundi la marafiki zako utaelewa maisha yako huenda umezungukwa na marafiki wanao kukatisha tamaa ya kufanya jambo zuri la manufaa,huenda umezungukwa na marafiki wanao kushauri vizuri lakini hawako tayari kukusaidia kufikia ndoto zako,huenda umezungukwa na marafiki wanao kupeleka mitandaoni kuzurura,huenda umezungukwa na marafiki wanao furahia kushindwa kwako.Amka ndugu ni kheri rafiki mmoja mwenye akili kuliko rafiki mia moja wapumbavu uwingi wao utakua kama makelele katika maisha yako kwasababu hamna jipya mtakalo shauriana na kulitendea kazi.

~TIMIZA MALENGO YAKO,unapokua tayari umepata shughuli ya kufanya jitahidi kuchunguza kwa undani kama shughuli hiyo inaweza kukutimizia malengo yako ambayo mengine ni ndoto za mafanikio unazo tamani kuzitimiza na kuziishi.Shughuli unayoifanya ndio inakujengea uhakika wa ndoto zako,usifanye shughuli inayokupa pesa ya kula tu na kuvaa,au kununua mafuta ya gari halafu ukarizika tafuta shughuli inayoweza kudumu kwako na kizazi chako nina maana kua utapokua mzee au umekufa wanao wajivunie jitihada zako za kuwakomboa kutoka umasikini,Hivyo malengo lazima yawe makubwa ili uongeze nguvu ya utafutaji,Kamwe usiweke lengo unalolizidi bali weka lengo linalokuzidi ili kulifikia uelewe unacho fanya na utajipima utendaji kazi wako.Hakikisha malengo yako yanatimia kwako na kizazi chako.

~UTAYARI WA KUSAIDIWA,usiwe mjuaji sana utakosa watu wa kukusaidia badala yake jishushe uelimishwe na usaidiwe ili uweze kufanya shughuli inayoweza kudumu kwako na kizazi chako,Ujuaji mwingi ni sumu kwa upeo wako kwasababu huenda unacho kijua hakina msaada kwako,jitahidi kua tayari kusaidiwa na wenzio katika mambo ya mafanikio.

JIFUNZE KUMTOLEA MUNGU,Mungu wetu anajaribiwa kwa sadaka na sio kitu kingine jiulize tangu uanze shughuli za kutafuta mafanikio umewahi kumtolea Mungu ile kumi ya mavuno? au hata sadaka umewahi kutoa? kutoa ni moyo unapotoa Mungu anarudisha mara kumi hivyo usiwe mchoyo hadi kwa Mungu,na unapotoa epuka kujitangaza wengi wanakosea akitoa sadaka basi anataka mtaa mzima wamuelewe,sadaka yako na iwe siri kati yako na Muumba wako.

Natumaini umepata wazo jipya kuhusiana na siri za mafanikio.Kwa ushauri wa kukusaidia shughuli za kufanya ufikie ndoto zako tuwasiliane��������

WhatsApp ……0673214813………

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni