Jumatatu, 18 Julai 2016

HISTORIA YANGU.

TIMIZA NDOTO ZAKO.

habari……………

naitwa Josinah Leonard Nzilayilunde,ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma(UDOM ) nikiwa nasoma shahada ya kwanza ya saikolojia ya watu wenye mahitaji maalumu(BA of education in special needs  ).

Kifamilia mimi ni mtoto wa kwanza ktk familia ya watoto wawili,familia yetu tunaishi na mama.Nikiwa kama binti mwenye kujipenda nilitamani sana kuwa na maisha mazuri,lakini kutokana na hali ya nyumbani kua ya kawaida nilijikuta ninavyo tamani haviendani na maisha yetu.Mara nyingi sana nilitamani kua na nguo nzuri zaidi,viatu,mikoba ya bei,gari la kutembelea na nyumba nzuri ya kuishi.lakini pia nilikua napenda kusaidia wahitaji ktk jamii yetu.

Nilianza biashara ndogo ndogo za kuuza nguo za mitumba,kuuza samaki,mihogo(vitafunwa ) na nilianza kucheza michezo ya upatu lengo ilikua ni kufikia ndoto zangu,lakini sikufika mbali kwani nilipata hasara sana.Muda huo nikihangaika hivyo nilikua nimemaliza kidato cha 4,hivyo matokeo ya kwenda kidato cha 6 yalikua mazuri hivyo nilianza masomo August 2013.

Nikiwa shuleni,nilijikuta natamani tena maisha ya wenzangu kwani walikua wanapewa pesa za kujikimu kwa upande wangu pesa ilikua chache hivyo sikua na ujanja zaidi ya kutulia tu,nikiwa bado shuleni nilianza biashara ya kuuza pipi na nguo za ndani za wadada pia urembo.Lakini bado sikufanikiwa.Hivyo nilimaliza kidato cha sita 2015,May

Baada ya kurudi nyumbani mambo yalizidi kua magumu kwani sikua na uwezo wa kumudu biashara yoyote kutokana na kukosa mtaji.Hivyo nilienda kukopa pesa kwa rafiki yangu nikaanza kuuza mihogo ya kukaanga,pia kupika uji.Hali hii iliniumiza sana kwani nilitumia muda mwingi sana bila faida niliyo itaka.Hivyo nilitamani hata kupata mwanaume wa kunihudumia.Haikua vizuri mimi kufanya hivyo japo sikuweza kupata mwanaume huyo hivyo nilipiga moyo konde na kuendelea na biashara zangu.kwasababu wanawake wengi wanapo shindwa kufanya shughuli zao wanakimbilia kutafuta wanaume.

Mnamo September 11 nilikutana na habari nzuri huko Facebook iliyokua inahusu fursa ya biashara ya mtandao(network marketing ) nilivutiwa sana na mfumo huo wa biashara,na sikusita kuanza biashara hiyo kupitia kampuni ya forever living.Kwa muda wa miezi 4 nilijipanga kupata mtaji kisha nikaanza biashara rasmi January 11 ya mwaka 2016.naweza kusema huu mwaka ni wa HABARI NJEMA.kwasababu fursa hii ya biashara imenipa mtazamo mpya.

1.Nimenufaika sana na afya,kwa kutumia bidhaa zenye ubora.mimi na familia yangu tumenufaika na afya.hatusumbuliwi tena na magonjwa kwani afya zetu ziko imara.


 2.Kupitia biashara hii nimejifunza kuwapenda watu walio fanikiwa ninawachukulia mfano ktk maisha yangu na safari ya mafanikio,hapo nyuma sikuwapenda matajiri kwasababu niliaminishwa kwamba wao wanakandamiza masikini kumbe sivyo,kupitia biashara hii nimejikuta napenda sana kujifunza kwa matajiri walio fanikiwa kwasababu wao pia walianza kama sisi,isipokua wao walibadili mtazamo na kujifananisha na washindi na hawakukata tamaa kufikia ndoto zao hata walipoanguka walisimama kuendelea na safari ya mamafanikio.kwangu mimi hii ni hatua kubwa sana.


3.Kupitia biashara hii nimejifunza uvumilivu kua na msimamo kwa ndoto zangu,naamini nitapata mafanikio makubwa kwasababu bado naendelea kujifunza lakini pia bado naendelea kuwaongoza wenzangu nao wafikie ndoto zao,naamini wenzangu wanapo fanikiwa kutokana na muongozo wangu ndipo hapo na Mimi nafanikiwa.hapo mwanzo nilifikiri kufanikiwa peke yangu tu kumbe sikua sahihi hivyo kupitia biashara hii nimejifunza upendo.

4.Kupitia biashara hii nimejifunza namna ya kutumia pesa,hapo nyuma nilikua nikitumia pesa bila mpangilio,sasa hivi ninaelewa maana ya akiba na kukuza uwekezaji kutokana na akiba ili niwe na mzungumko mzuri wa pesa,pia nimeamini kwamba ppesa inaweza kumtumikia mtu yoyote endapo tu utakua tayari kubadili mtazamo 

5.Kipato,fursa hii imenisaidia kutengeneza kipato kizuri,kupitia kipato ninacho pata sasa nimeanza kuamini kua mtu yoyote anaweza kufikia ndoto zake,kwa mwezi nimeweza kujikimu mahitaji madogo madogo kama binti lakini pia nimeweza kusaidia familia yetu kuweza kujenga nyumba ya kuishi,hivyo tumetoka ktk mazingira ya kupanga.lakini pia kipato hicho kinaongezeka siku hadi siku tofauti na ajira kwasababu mara nyingi mishahara haikutani,pia mshahara haupandi kwa walio chini.Hivyo naamini kupitia biashara hii ninakua milionea ndani ya miaka 5 tu.

6.kupitia biashara hii nimepata muongozo kwa wenzangu walio nitangulia ktk biashara hii kwa mafunzo mbalimbali,hii imeniondolea woga wa kuthubutu kwasababu nimeshikwa mkono.tofauti na biashara nyingine nimeona huku kuna umoja sana sana.Hivyo naona ni mahali salama kwangu na kwa mtu yoyote kutimiza ndoto zake.


7.Nimeweza kuwaongoza ndugu jamaa na marafiki kuweza kufanya biashara hii kwani ktk biashara hii tunasaidiana ili kila mtu kufikia malengo yake,hii ilikua ndoto yangu ya miaka mingi kusaidia watu kwa namna mbalimbali hivyo kupitia fursa hii naendelea kugusa maisha ya wengi,hivyo hata wewe unae soma ujumbe huu unaweza kwasababu tutakushika mkono.

8.Nimejifunza mambo mengi ambayo sikufundishwa shuleni,hasa swala la kutunza muda,kutunza pesa,kuwa kiongozi,kuongea na watu,nimepata mtazamo mpya juu ya mafanikio kwani hapo awali nilifikiri haiwezekani mimi kufanikiwa lakini kupitia fursa hii nimebadili sana mtazamo wangu juu ya mafanikio sasa ninaamini ktk mafanikio.

9.Kupitia biashara hii nimeweza kusafiri na naendelea kusafiri dunia,kwani kampuni yetu inatupa nafasi ya kusafiri angalau mara mbili kila mwaka kwenye nchi mbili tofauti.Hivyo safari hizi zinanijengea kujiamini pia kujifunza zaidi.

10.kupitia biashara nimejifunza mafanikio sio kwa wasomi tu,bali ni kwa kila mtu hata ambao hawajasoma kwasababu kitu cha kwanza kinacho onesha kua unahitaji mafanikio ni jinsi akili yako inavyo kubali,pia juhudi kwasababu nimeona wasomi wengi lakini bado maisha yao ni magumu,hivyo biashara hii imeniondolea matabaka ktk mafanikio,kufanikiwa ni kuiandaa kwanza akili kisha kuambatana na walio fanikiwa,kua tayari kusaidia hakika utajifunza mengi ambayo huwezi kuyapata darasani.

11.kupitia biashara hii nimeweza kupata marafiki wapya wenye mitazamo chanya ambao wananiongoza ktk hatua za mafanikio.Naamini nguvu ya marafiki wenye mtazamo chanya ktk safari ya mafanikio kwasababu marafiki walionizunguka ndio wanao tafsiri muonekano na mtazamo wangu,hivyo hii biashara kwangu imekuwa zaidi ya maisha.nimejifunza kumbe marafiki wanaweza kuchangia kufanikiwa kwangu hivyo naendelea kutazama marafiki wengi zaidi wenye mitazamo chanya ili niendelee kujifunza kutoka kwao.hata kwako wewe inawezekana angalia sana marafiki walio kuzunguka.

Hizo ni baadhi ya faida nilizo pata kutokana na biashara hii ya mtandao kupitia kampuni ya forever living.hivyo kwa kumalizia napenda kukutia moyo unaesoma story yangu amini kua inawezekana kubadili maisha yako hivyo kama unazo ndoto usisite kuzitimiza.

KUTANA NA FOREVER LIVING,IKUBADILISHE MAISHA YAKO.

JOSINAH LEONARD NZILAYILUNDE.

#0673214813……………WhatsApp

josinah.jl@gmail.com

Maoni 1 :

  1. UTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI

    (Kwanza kabisa nataka kukwambia kwamba hakika utajili ni azina kutoka kwa mwenyezi mungu na pia kuna viumbe alio wapa mamlaka na nguvu ya kumiliki mali)


    MPAKA MASAA 72(SIKU3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA

    kwa maelezo kamili piga namba +255742162843

    (KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
    (HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
    MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.

    NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.

    (kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
    1. uwe una umri wa miaka 18+
    2. uwe tayari kupokea masharti yote
    3.uwe na uwezo wa kutunza siri
    4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
    KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU.

    JibuFuta