Jumatano, 20 Julai 2016

JINSI DAKIKA MOJA INAVYOWEZA KUBADILI MAISHA YAKO.

Duniani kote,kila mtu ana miliki masaa 24 katika masaa hayo tunamgawanyiko mara tatu yani masaa 8 ya kufanya kazi,masaa 8 kulala na 8 kufanya shughuli za ziada.Tunapozungumzia muda ni dhahiri kua wengi wametawaliwa na muda badala ya wao kutawala muda.

unaweza kua unajiuliza ni kwa namna gani?

sasa sikiliza,kama wewe ni muajiriwa au umejiajiri mwenyewe unatakiwa kufuata utaratibu huu ili uweze kumiliki muda na sio muda ukumiliki.

>Panga ratiba yako ya shughuli za kila siku ambazo zinakuingizia kipato,Unapofanya shughuli bila ratiba ni wazi kwamba wewe si mwaminifu kabisa kwasababu hapo katikati anaweza kuja rafiki akakubeba mwende matembezi na ukakubali,inakua hivyo kwasababu huna ratiba yani wewe ni kanyaga twende.Sikiliza ratiba yako ndio inaamua wewe uwe mtu wa namna gani,hivyo ratiba huendana na muda.Unaona dakika moja ya kumkubalia rafiki mwende matembezi itakugharimu sana kuifidia kwasababu pengine ungebaki kwenye shughuli zako usingepata majanga ya kuibiwa au kuumizwa kutokana na majanga ya matembezi.ILINDE DAKIKA YAKO

2.Andaa muda wa kujifunza vitu vya mafanikio,watu wengi hawana muda wa kujifunza tangu alipo maliza chuo au form four hajawahi kujifunza tena.Elimu haina mwisho ndugu yangu labda nikupe siri moja wenzetu wazungu kwa siku wanatenga masaa 2 tu ili kujisomea vitabu au makala mbalimbali ambazo zinalenga kuwaongezea ujuzi ktk maisha.Ajabu huku kwetu Tanzania watu mko bize kusoma comments za matusi kwa wema sepetu,mko bize kutazama ngono,mko bize kujifunza ujambazi yani mambo yasiyo faa kabisa.Hebu tumia hiyo dakika moja kuilisha akili yako busara na maarifa ya maisha,halafu uone dakika hiyo itakavyo kubadili kabisa wewe utajikuta ni mtu mwenye utofauti na wale wasio na muda wa kujifunza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni